Uume (Penis) ni kiungo chenye hisia na muhimu katika jinsia ya kiume kutokana na nafasi yake katika mwili.

Wanaume wengi wamekuwa wakitumia kiungo hicho pasipo kuzingatia utunzaji wake nakuifanya sehemu hiyo nyeti kuwa chafu na hata pengine kutoa harufu mbaya kwa kutoifanyia usafi sawasawa hasa baada ya kushiriki tendo la ndoa na kusisahidia haja ndogo.

Leo kati safu hii ya afya nikakufahamisha jinsi 10 muhimu za kutunza uume wako:

Usafi kwa asiyefanyiwa Tohara

Watu wengi usahau hata kushindwa kusafisha ngozi ya juu ya Uume wakati wa kuoga na baada ya tendo la ndoa na hasa wale ambao bado wana Ngozi ya juu ya uume (govi) na kusahau kusafisha eneo la chini yake. Kama una ngozi ya mbele katika uume (govi), unapaswa kuvuta kwa chini kwa upole ngozi hiyo na kufua eneo la chini yake na maji moto. Kama utashindwa kufanya hivyo utasababisha eneo hilo kuwa na harufu mbaya na kusababisha kuzaliana kwa bakteria.

Kunawa mikono

Ni lazima kuwa na tabia ya kusafisha uume wako si tu baada ya kutoka chooni lakini pia kabla. Osha mikono yako wakati wowote kabla ya kugusa uume wako. Hii ni kutokana kushika vitu vingi ambapo kunakuwa na uwezekano mkubwa wa kutunza kemikali. Pia ni muhimu kama umekuwa katika kuwasiliana na watu hivyo uweza kubaki na chembechembe ambazo zinaweza kusababisha muwasho kwa kushika pilipili hivyo utajikuna na kusababisha michubuko katika uume.

Uchunguzi wa Mara kwa Mara

Si tu kama wanawake wenyewe ndio wanashauriwa kujitegemea kwa kufanyiwa uchunguzi wa saratani ya matiti na kizazi, Lakini pia wanaume wanapaswa kuwa na utaratibu wa kuangalia sehemu zao za siri kama wana uvimbe wowote na pia kwa ishara ya magonjwa ya zinaa. Kuchunguza pia shahawa yako kutambua mabadiliko yoyote katika muonekano au uwepo wa damu katika uume.

Epuka Majeraha

Uume wako unahitaji ulinzi, upendo na huduma kutoka kwako sambamba na kuepuka hali ambazo zinaweza kusababisha majeraha katika uume. Hii inaweza kutokea kwenye ngono isiyo salama au punyeto bila kurainisha ngozi. Pia kuhakikisha unaepuka kuvaa nguo ya ndani (chupi) ambayo haibani sana. Ni vyema ukapata muda wa kukaa bila nguo ya ndani (chupi) ili kuweka wazi uume na kuepusha msuguano utakaoweza kuleta madhara.

Kuwa na mwanamke mmoja

Kuwa na mpenzi zaidi ya mmoja uua uwezo wako kingono lakini pia kuwa na mwanamke mmoja kutakusaidia kuwa mwenye tabia njema na kuwa na nguvu na uwezo mzuri wakati wa kufanya tendo la ndoa na hasa kabisa kujikinga na magonjwa ya zinaa.

Kupata muda wa Mapumziko

Hii ni nzuri kwa afya yako kwa ujumla lakini nzuri hasa kwa uume wako kuwa na afya. Kila wakati kila unapokuwa umepumzika kwa usingizi mzito, uume wako utakuwa na uimara kutokana na kuupumzisha. Hii ni muhimu kwa sababu husaidia kurejesha sura yake na pia kuongeza muda wa utendaji kazi wa damu yenye oksijeni.

Kunywa maji

Kuwa na tabia ya kunywa angalau glasi nane za maji safi. Maji huvuta sumu nje ya mwili wako na kuruhusu damu kufanya kazi na kuongeza kukusisimua wakati wa tendo la ndoa.

Uchaguzi wa sabuni ya Kuogea na mafuta

Ni vizuri na muhimu kufanya usafi wa sehemu za uzazi. Na hata hivyo haipaswi kwenda kuosha na kuskrabu sehemu za siri kwani ngozi ya uume ni raini na nyeti. Matumizi ya sabuni ambazo uondoa vidonda si nzuri kwa kutumia katika uume na kwa kutumia kama njia ya kurainisha uume wakati wa tendo la ndoa lakini pia ni kivutio cha maambukizi. Vizuri kuosha mara mbili kwa siku na maji ya joto kwa kutumia sabuni za kawaida.

Kwa nini unapaswa kunyoa


Mwanaume unaweza kutoona umuhimu wa kunyoa kama ilivyo kwa mwanamke lakini ukweli ni kwamba hata wewe unapaswa kunyoa na kutumia nyia nyepesi za kunyoa ili kuweka eneo lako la uzazi laini na safi. hivyo kama kunyoa mwenyewe kutakuwa na kisingizio mnaweza kufanya hivyo pamoja kama wanandoa hivyo mwenza wako akakuweka katika hali ya usafi.


Moja ya gumzo kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa ni uwepo wa video fupi inayomuonesha mwananke anayedaiwa kuwa mchawi baada ya kukutwa katikati ya barabara akiwa bila ungo na baadhi ya vitu vinavyodhaniwa vya kishirikina.
Sasa new stori leo leo July 20, 2017 kwenye Hekaheka ya Leo Tena ya Clouds FM mtangazaji Geah Habibu katusogezea hii iliyotokea Kipunguni ambako mwanamke mmoja mwenye mume na watoto alikutwa katikati ya barabara akiwa bila nguo kwa kinachodaiwa ni maelekezo ya Mganga.
Tukio hilo limetokea July 18, 2017 majira ya saa sita mchana ambapo baada ya kukutwa katika hali hiyo wananchi walidhani ni mchawi na wakadhamiria kumchoma moto lakini aliokolewa na Polisi baada ya taarifa kumfikia Mwenyekiti wa eneo hilo…sikiliza full stori kwa kuplay hapa!!!

Moja ya headlines zinazomuhusu mwimbaji sataa wa Bongofleva kutoka kundi la Yamoto Band, Beka Flavour leo July 20, 2017 ni kuhusu kushikiliwa kwake na Jeshi la Polisi DSM kwa mahojiano yaliyodumu kwa saa Tisa kuanzia saa tano Asubuhi hadi saa mbili Usiku.
Ayo TV na millardayo.com zimempata Beka Flavour>>>”Nipo hapa tangu saa tano Asubuhi kwamba natuhumiwa kutapeli pesa za jamaa mmoja kupitia mitandao yangu ya kijamii. Huyu jamaa anaishi Kigoma na anadai kuwa alikuwa akizungumza na mimi na anasema hakuwahi kuonana na huyo Beka basi nilipata taarifa a kuripoti katika kituo hiki na niliporudi kutoka Safari ndio nimelifika hapa.
“Nimetoka kwa dhamana na kikubwa ningependa kuwaomba watu na mashabiki wengi kwamba watu wanaotumia majina yetu sio kitu kizuri kwani kama huyo wa Kigoma aliyetuma pesa anadai ametuma zaidi ya milioni 8. Kwa hiyo, wawe makini na mitandao feki kwani Maromboso, Enoki na wengine hatuna kurasa za Facebook.” – Beka Flavour.
“Kwa sasa nina Manager mpya mbali na Yamoto Band” – Becka Flavour…PLAY kwenye hii VIDEO kutazama kila kitu!!!




Kuna wanawake kadhaa huwa wanafurahia sana kuwa wao kila wanapopita wanaume wanawatongoza. wanaongea kwa majidai sana na furaha kama vile ni jambo la kujivunia.

Ukweli ni kuwa mwanamke ukiona unatongozwa kila sehemu na kila mwanaume ujue wewe ni kimeo sana. sana yaani kila mtu anaona kuwa ana uwezo wa kukupata. unakuwa kama vile daladala au bodaboda kila mwenye uwezo wa kusimamisha anasimamisha. ni kuwa upo kiwango cha kuwa used anytime na anybody. so epuka hali inayokufanya uonekane cheap.

usifurahie kuwa kila unapopita watu wanapiga miluzi na kukufurahia wakikuita ukaona kuwa una nyota ya kupendwa. ujue una nyota ya mbwa kupigiwa miluzi au nyota ya uchafu kufuatwa na inzi. haiwezekani kila mtu anakusimamisha kukutaka kimapenzi. muuza maji, dereva wa boda boda, dereve wa daladala. dereva taxi, jamaa tu njiani kakuona, mwanasheria,ukienda hosp dokta anakutaka, nurse naye anakutaka, ukienda shule mwalimu naye anakutongoza. ukienda ofis flan hr naye anakutaka, mlinzi naye...

yaan wewe unatakwa na kutongozwa na kila mwanaume hapa duniani kasoro tu wale wenye kujiheshimu sana ingawa nao ukiwa kalia maeneo yao ya siri nao wanakugagadua. halafu unajisifu kwa wenzio kuwa wewe unapendwa sana na wanaume una mvuto.... hata uchafu nao husema una mvuto kwa kuwavutia inzi na wadudu wengine kama funza,kunguru n.k
Mapema leo kulikuwa na stori kuwa TRA Mwanza imeifungia Kampuni ya Sahara Media inayomiliki Star TV, RFA na Kiss FM wakiidai malimbikizo ya kodi ya zaidi ya Tsh. Bilion 4 wakiitaka kulipa ndani ya siku 14 vinginevyo kampuni itapigwa mnada.
Baada ya taarifa hizo Meneja Rasilimaliwatu wa Sahara Rafaeli Shilatu amekiri kufungiwa akidai ni kutokana na malimbikizo ya kodi baada ya uwekezaji mkubwa waliofanya wakati wa kuhama kutoka analogy kwenda Digital ingawa wanajitaidi kuhakikisha kwamba wanarudi hewani na kulipa kodi kama kawaida.
>>>”Lazima tukiri kwamba mmeshuhudia TRA wamefunga maeneo yetu ya kazi na hii inatokana na malimbikizo ya kodi ambayo siyo ya sasa ni ya muda mrefu hata nyie waandishi wa habari mnajua kwamba kadri uwekezaji unavyokuwa mkubwa ndivyo gharama zinazidi kwenye uwekezaji. So, ilitulazimu kutafuta fedha kwenye mabenki ili tuweze kukidhi matakwa ya Serikali ya kuhama analogy kwenda Digatal.
“Niwatoe wasiwasi Watanzania na wapenzi wa Sahara hili ni jambo la muda lakini kampuni yetu inafanya jitihada kuhakikisha kwamba haya yanamalizika vyombo vyetu virudi hewani.” – Rafaeli Shilatu 
Bonyeza Play hapa chini kusikiliza Full story. Source http://millardayo.com/



Kuna watu wanna Mikwara sana, ukiachana nae anaanza Maneno ya shombo, wengine hudiriki kukwambia ''you cant live without me utarudi tu'', unajiuliza huyu mtu ana Hisa kwenye mishipa yangu ya moyo au ana mrija wa Oxygen yangu ya kutumia kesho?? Kama nilizaliwa peke yangu kwanini nisiweze kuishi wewe ukiondoka??

Maneno ya mkosaji haya, usiyasikilize kamwe! Unapoamua kufanya Maamuzi magumu usisikilize kingine chochote, Follow your heart. Wengi wamegeuzwa watumwa kwa kuamini they cant live bila watu fulani, kisa wamezoeana, au wamekaa muda mrefu kwenye mahusiano, unahisi kama hutaweza... Hamna kitu kisichowezekana, Mungu ameumba kusahau, utapona maumivu na utasonga! Hakuna destiny rahisi ya Kimapenzi bila kufanya maamuzi magumu, lasivyo Jiandae kuwa mtumwa wa mtu fulani, binadamu fulani ambaye naye amegundua wewe ni dhaifu na anatumia udhaifu wako kukutesa maisha yote...

Amua leo, Uwe mtumwa wa mtu au utengeneze furaha yako kwa Kumove on kupata Lover of you life




















ROMA MKATOLIKI: SIKUTEKWA KWA SABABU ZA MZIKI

Tuesday 11 July 2017
Posted by Unknown
Tag :
Mwanamuziki Ibrahim Mussa ‘Roma Mkatoliki” amesema kuwa tukio lililotokea miezi mitatu iliyopita lilikuwa na sababu nyingine zaidi ya muziki anaoufanya, tofauti na watu wanavyodhani.

Roma aliyasema hayo katika mahojiano na EATV kwamba alijua kuwa atawakwaza baadhi ya watu kwa kutosema na kuweka wazi mambo kadhaa kuhusu tukio hilo ikiwemo kutekwa, walipopelekwa, kilichowatokea wakiwa huko walikopelekwa n.k lakini aliamua kutumia busara na kutosema kitu ili aweze kulinda sanaa na maisha yake kwa ujumla.

“Mimi najua nini kilipelekea wale jamaa kututeka. Ni zaidi ya muziki, japo chanzo ni muziki ndio maana walikuja kututeka tukiwa studio na si kanisani wala nyumbani. Unajua wananchi tayari walikuwa na video kichwani wakijua Roma anakuja kuongea hiki na kile, tunamaliza pale halafu usiku mwema.”

“Lile tukio lilikuwa linahitaji busara ili maisha yaweze kuendelea. Labda ningesema ukweli pengine ungekuwa ndio mwisho wa Roma kwenye muziki. Mashabiki wangeshangilia lakini kwa wadau mbalimbali mchango ndio ungekuwa umekwisha,” alisema.
Roma alisisitiza kuwa kama angeweka wazi jambo hilo siku ile ambayo alitoka, ingepelekeaa yeye kuacha muziki na kurudi Tanga kufanya mambo mengine, kwani hakuna mtu ambaye angetaka kuwa karibu naye tena.

“Toka nimetoka mpaka sasa sitaki kutazama video mbalimbali ambazo zinaonesha jinsi watu walivyokuwa wakihangaika kututafuta. Sitaki kutazama kwa sababu sitaki kukumbuka kabisa hali ambayo nilikuwa nayo kipindi kile. Pia sipendi kabisa kuona mtu mwingine yeyote anakwenda huko chimbo ambako tulikuwa tumewekwa tukipata mateso,” alisema.

Roma na wenzake walitekwa mwezi wa nne mwaka huu walipokuwa katika studio za kutayarisha muziki za Tongwe Records na kupelekwa kusikojulikana kwa muda wa siku tatu na kuja kuonekana wakiwa na majeraha mbalimbali mwilini.


  


Leo June 21, 2017 kupitia XXL ya Clouds FM Mwimbaji staa wa Bongofleva Diamond amezungumzia kwa mara ya kwanza tangu kupost picha na ujumbe kwenye Instagram yake juu mama watoto wake ‘Zari’ kufuatia picha aliyopiga akiwa na mwanaume akiogelea.
Diamond amesema baada ya kuiona picha hiyo alipanic na kuandika ujumbe ule ambao baada ya kusambaa alifuatwa na Zari na alipomuelewesha alimuelewa huku baadhi ya mastaa wa Afrika wakiwepo P Square na Fally Ipupa wakimpigia simu kumpoza hasira.
>>>“Mara ya kwanza nilipoona picha ya Zari kapiga na mtu kwenye maji nilipanic na nilichokiandika kwenye insta yangu nilimaanisha. Baada ya post yangu ya insta wasanii wengi walinipigia simu. P Square na Fally Ipupa walinicheki. Zari baada ya kuona post yangu Insta alikuwa ofisini, alirudi nyumbani na aliponielewesha nilikuwa mpole.” – Diamond Platnumz.
ULIPITWA: Majibizano ya Diamond Platnumz na Zari 

Bonta Maarifa Ft Barakah The Prince - Zero.mp3

Friday 14 April 2017
Posted by Unknown
Tag :

 Bonge La ngoma Najua kama unapenda Hip Hop Lazima hii ngoma utaikubali tu kutoka kwa 
 Bonta Maarifa Ft Barakah The Prince - Zero.mp3


 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ameviagiza vyombo vyote vya ulinzi na usalama kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kuhakikisha vinasimamia sheria ipasavyo ili kukabiliana na tatizo hilo hapa nchini.

Mhe. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 12 Februari, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kuwaapisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Rogers William Siyanga, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mhe. Joseph Edward Sokoine, Balozi wa Tanzania nchini Algeria Mhe. Omar Yusuf Mzee na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Grace Aaron Mgovano.

Mhe. Dkt. Magufuli amewataka viongozi wote wa Serikali kuungana na vyombo vya dola katika mapambano dhidi ya watu wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya na ametaka mapambano hayo yasifanywe kwa mzaha wala kwa kuangalia majina ya watu, vyeo vyao na taasisi wanazoongoza.

Mhe. Rais Magufuli amewapongeza viongozi wote wa mikoa walioanza kukamata watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na amewaomba Watanzania wote waunge mkono juhudi za kukabiliana na wanaofanya biashara na kutumia dawa za kulevya ambazo zinazidi kuangamiza nguvukazi ya Taifa.

“Niwaombe ndugu zangu tuungane katika vita hii dhidi ya dawa za kulevya, waandishi wa habari na wana mitandao tuweke mbele Utanzania wetu, akitokea mtu anapambana na dawa za kulevya tumuunge mkono badala ya kumchafua.

“Vita hii ni kubwa hatuwezi kwenda nayo kwa mzaha na Serikali itahakikisha inasimamia sheria namba 5 ya mwaka 2015 iliyohusu kuzuia na kupambana na dawa za kulevya ambayo ilitungwa na Bunge la 10 lililoongozwa na Spika Anna Makinda na sheria hiyo ikatiwa saini na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, nawapongeza sana kwa kutunga sheria hii.” Amesisitiza Mhe. Rais Magufuli

Pia, Mhe. Dkt. Magufuli amesema takwimu zinaonesha kuna watanzania 1,007 wamekamatwa na kufungwa gerezani katika nchi mbalimbali baada ya kupatikana na makosa ya kujihusisha na dawa za kulevya, na amemuagiza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mabalozi wote wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi hizo kutojihusisha kuwatetea waliofungwa kwa makosa hayo na badala yake waache sheria za nchi husika zichukue mkondo wake.

Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemtaka Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala kufanya mabadiliko makubwa ndani ya Idara ya Uhamiaji nchini kutokana na utendaji wake kutoridhisha.

“Nataka ukafanye mabadiliko makubwa (Total Reform), nataka Uhamiaji izalishe fedha kwa ajili ya nchi hii, nataka ukadhibiti utoaji hati za kusafiria (Passports) maana zimekuwa zikitolewa hovyohovyo” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.

Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao pamoja na kula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela, imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Kaimu Jaji Mkuu Mhe. Prof. Ibrahim Juma, Mawaziri, Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama.

Gerson Msigwa

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU

Dar es Salaam

12 Februari, 2017

Miezi kadhaa baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kupiga marufuku biashara ya Shisha kwenye sehemu za starehe, ulipita muda na agizo hilo likaonekana kutekelezwa japokuwa haikuchukua muda sana biashara hiyo ikarejea tena.
November 16, 2016 wakati wa uzinduzi wa mitambo ya ufuaji umeme jijini Dar es salaam, Paul Makonda alizungumzia biashara hiyo kurejea kinyemela ikiwa ni pamoja na baadhi ya wafanyabiashara kumfata na kutaka kumuhonga shilingi milioni tano ili wapewe kibali cha kuendelea na biashara hyo.
Makonda amesema kurejea kwa biashara hiyo kunampa mashaka kwamba huenda baadhi ya askari wa jeshi la polisi wamepokea hizo pesa ndiomana wanashindwa kuzuia uuzwaji wa shisha.
Kauli ya  Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda imefanya Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamanda Simon Sirro kutolea majibu kuhusu biashara ya Shisha inayofanyika pamoja na kupigwa marufuku.
“Watu wengi wameshakamatwa pale Oysterbay na majalada yanaandaliwa na mengine yameshapelekwa kwa mawakili wa serikali. Sisi tunaendelea na oparesheni kama kawaida ya kukamata wauzaji, watengenezaji na wavutaji wa shisha” – Kamanda Sirro
Unaweza kutazama video hii kupata majibu ya jeshi la polisi.

NUKUU ZA RAIS JOHN POMBE MAGUFULI-04

Thursday 8 September 2016
Posted by Unknown
Tag : ,



counter




























Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, ni kiongozi ambaye watanzania tulikuwa tunamsubiri kwa muda mrefu.Mara nyingi anapohutubia huwa anatoa kauli za kufurahisha kwa wapenda maendeleo na kuchukiza wasiopenda maendeleo.
Mtandao huu unakuletea Nukuu za Rais, ambazo zinafurahisha wengi na kuchukiza wachache.





NUKUU 

"Nataka niwaeleze ndugu zangu, serikali hii ya awamu ya tano ipo pamoja nanyinyi, haitowatupa wala haitowabagua, haitowabagua kwa dini zenu haitowabagua kwa makabila yenu na kamwe haitowabagua kwa sababu ya vyama vyenu." 

MAANA YAKE 

Serikali ipo kwa ajili ya kutenda haki kwa raia wote bila kujali dini, kabila au vyama.

Maneno hayo alisema Magomeni, alipowatembelea wakazi waliokuwa wakiishi magomeni kota. Jumanne,06 Septemba, 2016.  

MUANDAAJI. NASSIR BAKARI
OFISI NDOGO ZA CCM
LUMUMBA 
EMAIL: nassiribakari@gmail.com 


tazama video chini  >>>>>>>>>>>>>>





Kamapa  kampa tena kijana Mahili REGGY THE BEST FT KIMBUNGA MCHAWI huwezi kuungalia Mara moja lazima utaurudia tu tena na tena  hebu ipakue uitazame

Welcome to My Blog

Popular Post

Blogger templates

About views Blogger

Mrembo wetu wa leo

KONA YA KIJANJA YA KUJIDA VIA SNAPS

Powered by Blogger.

MY HOT BROGGER TZ

Like My Facebook Page

FOLLOW ME ON TWITTER

Contact Form

Name

Email *

Message *

- Copyright © TIMOKUCHAZ -Robotic Notes- Powered by Blogger - Designed by Johanes Djogan -