Showing posts with label NEWS. Show all posts
DSM haiishi vituko…gumzo la Mwanamke aliyekutwa bila nguo barabarani
Saa 9 za Beka Flavour kukaa Kituo cha Polisi…adaiwa kutapeli Tsh. Milioni 8.9
Walichokizungumza Star TV baada ya kufungiwa na TRA
Mjadara baada ya Mbunge wa Sengerema Mhe. William Ngeleja kurudisha Fedha za Mgao wa Escrow
“Nilipanic nilichokiandika Insta kuhusu Zari” – Diamond
Rais Magufuli aviagiza vyombo vya ulinzi na usalama kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, ameviagiza vyombo vyote vya ulinzi na usalama kuongeza nguvu katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya kwa kuhakikisha vinasimamia sheria ipasavyo ili kukabiliana na tatizo hilo hapa nchini.
Mhe. Rais Magufuli ametoa agizo hilo leo tarehe 12 Februari, 2017 Ikulu Jijini Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kuwaapisha Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya Bw. Rogers William Siyanga, Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala, Balozi wa Tanzania nchini Ubelgiji Mhe. Joseph Edward Sokoine, Balozi wa Tanzania nchini Algeria Mhe. Omar Yusuf Mzee na Balozi wa Tanzania nchini Uganda Mhe. Grace Aaron Mgovano.
Mhe. Dkt. Magufuli amewataka viongozi wote wa Serikali kuungana na vyombo vya dola katika mapambano dhidi ya watu wanaojihusisha na biashara haramu ya dawa za kulevya na ametaka mapambano hayo yasifanywe kwa mzaha wala kwa kuangalia majina ya watu, vyeo vyao na taasisi wanazoongoza.
Mhe. Rais Magufuli amewapongeza viongozi wote wa mikoa walioanza kukamata watu wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na amewaomba Watanzania wote waunge mkono juhudi za kukabiliana na wanaofanya biashara na kutumia dawa za kulevya ambazo zinazidi kuangamiza nguvukazi ya Taifa.
“Niwaombe ndugu zangu tuungane katika vita hii dhidi ya dawa za kulevya, waandishi wa habari na wana mitandao tuweke mbele Utanzania wetu, akitokea mtu anapambana na dawa za kulevya tumuunge mkono badala ya kumchafua.
“Vita hii ni kubwa hatuwezi kwenda nayo kwa mzaha na Serikali itahakikisha inasimamia sheria namba 5 ya mwaka 2015 iliyohusu kuzuia na kupambana na dawa za kulevya ambayo ilitungwa na Bunge la 10 lililoongozwa na Spika Anna Makinda na sheria hiyo ikatiwa saini na Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, nawapongeza sana kwa kutunga sheria hii.” Amesisitiza Mhe. Rais Magufuli
Pia, Mhe. Dkt. Magufuli amesema takwimu zinaonesha kuna watanzania 1,007 wamekamatwa na kufungwa gerezani katika nchi mbalimbali baada ya kupatikana na makosa ya kujihusisha na dawa za kulevya, na amemuagiza Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Mabalozi wote wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi hizo kutojihusisha kuwatetea waliofungwa kwa makosa hayo na badala yake waache sheria za nchi husika zichukue mkondo wake.
Wakati huo huo, Mhe. Rais Magufuli amemtaka Kamishna Jenerali wa Uhamiaji Dkt. Anna Peter Makakala kufanya mabadiliko makubwa ndani ya Idara ya Uhamiaji nchini kutokana na utendaji wake kutoridhisha.
“Nataka ukafanye mabadiliko makubwa (Total Reform), nataka Uhamiaji izalishe fedha kwa ajili ya nchi hii, nataka ukadhibiti utoaji hati za kusafiria (Passports) maana zimekuwa zikitolewa hovyohovyo” amesisitiza Mhe. Rais Magufuli.
Hafla ya kuapishwa kwa viongozi hao pamoja na kula kiapo cha uadilifu kwa viongozi wa umma kilichoongozwa na Kamishna wa Maadili Mhe. Jaji Mstaafu Harold Nsekela, imehudhuriwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Kaimu Jaji Mkuu Mhe. Prof. Ibrahim Juma, Mawaziri, Makatibu Wakuu wa Wizara mbalimbali na Wakuu wa vyombo vya Ulinzi na Usalama.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
12 Februari, 2017
Mtandao huu unakuletea Nukuu za Rais, ambazo zinafurahisha wengi na kuchukiza wachache.
NUKUU
"Nataka niwaeleze ndugu zangu, serikali hii ya awamu ya tano ipo pamoja nanyinyi, haitowatupa wala haitowabagua, haitowabagua kwa dini zenu haitowabagua kwa makabila yenu na kamwe haitowabagua kwa sababu ya vyama vyenu."
MAANA YAKE
Serikali ipo kwa ajili ya kutenda haki kwa raia wote bila kujali dini, kabila au vyama.
Maneno hayo alisema Magomeni, alipowatembelea wakazi waliokuwa wakiishi magomeni kota. Jumanne,06 Septemba, 2016.
MUANDAAJI. NASSIR BAKARI
OFISI NDOGO ZA CCM
LUMUMBA
EMAIL: nassiribakari@gmail.com
Kilichoandikwa na mashabiki wa Ex wa Zari, Ivan baada ya kum-wish Tiffah
Zai
Mmoja kati ya watu ambao wamem-wish binti huyo ni Ex wa Zari, Ivan ambapo amemtakia binti huyo afya njema katika maisha yake. Lakini ujumbe huo umezua upya vuguvugu kwa mashabiki ambao bado wanaamini Tiffah ni mtoto wa Ivan licha ya Diamond kukanusha uvumi huo mara kadhaa.
“Big shoutout to this innocent beautiful soul. May you live to blow more candles to come Princess_tiffah,” aliandika Ivan katika ukurasa wake wa instagram huku akiwa ameweka picha ya binti huyo.
Baada ya kuandika ujumbe huo, mashabiki katika mitandao ya kijamii wamekuwa na maoni tofauti. Haya ni baadhi ya maoni ya mashabiki hao.
Mtoto karudi kwa baba jaman, Damu nzito nyie @ivandon ongera Ivan kwakupigania mpaka mwanao kaja atimaye mungu mkubwa jaman khaa.
Sweet_verosa
Hahaha yani nimecheka mpaka nimelia eti Mungu mkubwa tifa karudi kwa baba yake.
Didiz_buu
Nimempenda Bure uyu mzungu wa kiganda sijui kisauz…. Big up bro Ivan…. U gat a unique heart… Happy birthday baby teepher
Angellyamuya
Congratulation big Boss I salute you.
Aniveraaaaa
Ivan Don Kai u re a man,dis jst gt me crying a u re a nice man.God will perfect everything dat concerns u and gve h a better companion amen.
Nelyhassan
Sure she is beautiful innocent soul happy birthday girl @princess_tiffah
Cassandra_jolly
Happy birthday to her…..u r a gentleman Ivan
Johnson_willo
Now i realize how gentle ur.@ivandon conglatulation men.And happybornday to the one and only.@princess_tiffah.
Binti_wa_bagoka
My love @christinamboy aiseeee njoo umuone mume wa zari alivyo zungu ametishaaaa
Chibogoyo alisema jana kuwa taasisi hiyo inataka kurudisha maadili na uzalendo kwa wananchi kuheshimu alama za Taifa.
Alisema watendaji wanaopeperusha bendera zilizochakaa na kupauka wanafanya makosa kwani kunaidhalilisha Serikali kwa kuwa mpya zinapatikana bila ya urasimu.
“Baadhi ya watendaji wamekuwa wakiacha bendera zinapeperuka hadi usiku wakati sheria inataka zishushwe saa 12.00,” alisema.
Alifafanua kuwa wananchi wanatakiwa kusimama kwa utulivu wakati bendera ya Taifa inapopandishwa na kushushwa.
“Tofauti na zamani, siku hizi bendera ya Taifa inapopandishwa watu wanapita na kupiga kelele kama vile hakuna jambo linalotokea,” alisema.
Kuhusu wimbo wa Taifa, Chibogoyo alisema haupaswi kuimbwa kwenye vilabu vya pombe bali kwenye mikusanyiko rasmi ya kiserikali.
“Huu siyo wimbo wa kuimbwa ovyo, lazima turudishe maadili yetu Watanzania,” alisema.
Mpigachapa huyo alisema viongozi, watendaji na wananchi wanatakiwa kujifunza na kuufahamu wimbo huo na kuonyesha hisia za kizalendo kwa nchi.
News Meya wa Kinondoni Atumbua Majipu Kwa Kufuata Taratibu Sio Misifa Kama Wale
Watumishi wa 4 afya wamefukuzwa kazi kwa utoro na rushwa, watumishi 3 uhandisi wamekutwa na hatia kwa kushushwa vyeo na madaraja na mtumishi wa fedha na biashara amepewa onyo kali
uamuzi kwa wahandisi umetokana na wao kushindwa kutumia taaluma zao vizuri kwenye ujenzi wa barabara.
watumishai hao walichukuliwa hatua baada ya kufunguliwa mashtaka, kufanyiwa uchunguzi wa tuhuma zao na wao kupewa muda wa kujitetea.
Baraza la madiwani limewapandisha vyeo watumishi 372, kuwabadilisha vyeo watumishi 9, na kuwathibitisha kazini watumishi 206 ambao walimaliza vipindi vya majaribio na kuonekana kuwa wanafaa kuwa watumishi wa umma
Nawapa hongera kwa kufanya kazi hii kwa weledi na sio kwa show off, wanaofanya kazi kwa show off ili kuonekana wanafanya kazi na wanapenda haki kumbe wana sura mbili wangeiga mfano huu
VIDEO:
PETE YA UCHUMBA (WALTER RWABUKAMBALA vs VIRGINIA CHIDYAKA picha ziko hapa>>>>>>>>>>>
Kama hukupata nafasi ya kujua hii baasi kaa ukijua WALTER RWABUKAMBARA ameshamvisha pete VIRGINIA CHIDYAKA
Sasa wako mbioni kuanzisha Family taarifa niliyonayo kwa sasa vikao vinaendelea na michango inaendelea kutolewa
Kama ungependa kuwachangia ili wafanikishe zoezi hili jema wasiliana na Llewellyn Mark kwa namba hizi 0713 697 043
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Christopher Fuime amesema tukio hilo lilitokea majira ya saa mbili usiku huu na chanzo cha mauaji hayo hakijafahamika.
“Tukipata chanzo itakuwa tayari upelelezi wetu umetimia, hivyo kwa sasa tunalifanyia kazi ili kubaini wahusika wa mauaji hayo,” amesema Fuime.
Video: Diamond Anyesha Mvua ya Hela Kwenye Birthday ya Mtoto wa Aunty Ezekiel
Aunty Ezekiel alitamani angeenda na mwavuli kujikinga na mvua ya hela iliyomnyeshea juzi kwenye birthday ya kutimiza mwaka mmoja ya mtoto wa Aunty Ezekiel na Mose Iyobo. Ni Diamond ndiye aliyesababisha mafuriko ya noti yaliyomfanya muigizaji huyo apagawe! Check video hiyo ujionee mwenyewe.
Haya Hapa Majina Ya Kambi Zote 11 Ya Wanafunzi Kidato Cha 6 Waliopangiwa JKT 2016
2.Mafinga Jkt .....<<bonyeza Hapa>>
3.Makutupora Jkt.......<<bonyeza Hapa>>
4.Mtabila Jkt......<<bonyeza Hapa>>
5.Kanembwa Jkt.....<<bonyeza Hapa>>
6.Bulombora Jkt.....<<bonyeza Hapa>>
7.Ruvu Jkt.......<<bonyeza Hapa>>
8.Mgambo Jkt ......<<bonyeza Hapa>>
10.Mlale Jkt.....<<bonyeza Hapa>>
11.Msange Jkt.....<<bonyeza Hapa>>
VIDEO: Kazi inaendelea na matunda yanakuja, Harmonize kazawadiwa gari na WCB
Kama nikusiivyo siku zote ni juhudi na Nidhamu yako ndio itayokufanya upate matunda ya kazi yako….. Usiache unyenyekevu, kuheshimu mkubwa na Mdogo, Kumuomba na kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kila hatua ndogo Uipigayo…. Congrats kwa your New Ride’ – Diamond