Showing posts with label MICHEZO. Show all posts

Usiku wa July 28 klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji inayochezewa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta ilishuka tena dimbani kucheza mchezo wake wa kwanza wa round ya pili wa kuwania kucheza hatua ya makndi ya Kombe la UEFA Europa League dhidi ya Cork City ya Ireland.

Mchezo wa kwanza wa round ya pili ya Europa League KRC Genk wameanzia katika uwanja wao wa nyumbani wa Cristal Arena wenye uwezo wa kuchukua mashabiki zaidi ya 24000 na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na mjamaica Leon Bailey dakika ya 31 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa mshambuliaji wa Kigiriki Nicolaos Karelis.
photonews-10594383-042-jpg_1469705623
Hata hivyo licha ya KRC Genk kupata ushindi huo wakiwa pamoja na nyota wao kutoka Tanzania Mbwana Samatta, bado wana wakati mgumu katika mchezo wa marudiano watakaocheza August 4 Ireland, kwani watakuwa wanahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ile ili waweze kusonga mbele katika hatua inayofuata na kuitoa Cork City.

Kama utakuwa unakumbuka vizuri KRC Genk wamekutana na Cork City, baada ya kuitoa Buducnost ya Montenegro kwa mikwaju ya penati 4-2, baada ya mechi yao ya mwisho kumalizika kwa Buducnost kuibuka na ushindi wa goli 2-0 ila kutokana na kuwa na aggregate ya 2-2 walilazimika kucheza dakika 120 na baadae mchezo ukaamuliwa kwa mikwaju ya penati.
June 24 Lionel Messi anakumbuka siku yake ya kuzaliwa, leo June 24 2016 anatimiza umri wa miaka 29, Lionel Messi ameweka rekodi nyingi katika soka ikiwemo ya kutwaa Ballon d’Or mara 5. Mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee mambo matano kuhusu Lionel Messi leo katika kumbukumbu yake ya kuzaliwa.

1- Mechi amecheza juml ya mechi 643.
2- Amefanikiwa kufunga jumla ya magoli 508.
3- Ametoa assist 213.
4- Ameshinda jumla ya mataji 28 katika soka.
5- Lionel Messi amefunga zaidi ya hat-trick  30 katika soka.


 

GOAL AND HIGHLIGHTS: MO BEJAIA VS YANGA JUNE 20 2016, FULL TIME 1-0


Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars March 23 imeshuka katika dimba la Idriss Mahamat kucheza na wenyeji wao timu ya taifa ya Chad katika muendelezo wa michezo ya makundi ya kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika  (AFCON) itakayochezwa mwaka 2017.

Huu ulikuwa ndio mchezo wa kwanza wa Mbwana Samatta akiichezea Taifa Stars kama nahodha wa timu hiyo, katika mchezo huo uliochezwa Chad, Taifa Stars imeibuka na ushindi wa goli 1-0, goli la Taifa Stars lilifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 30, baada ya kutumia vyema krosi ya Farid Musa.

Samatta amefanikiwa kuitunzia Tanzania rekodi dhidi ya Chad, kwani mara ya mwisho Taifa Stars alikutana na Chad, ugenini na kufanikiwa kuibuka kwa ushindi wa goli 2-1. Magoli ya Taifa Stars wakati huo yalifungwa na Mrisho Ngassa dakika ya 11 na Nurdin Bakari dakika ya 88, huku goli la Chad la kufutia machozi lilifungwa na Mahamat Labbo dakika ya 12.
raaaa
Msimamo wa Kundi G ulivyo hadi sasa
Taifa Stars itarudiana na Chad Jumatatu ya March 28 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, huku ikiwa imebakiza mechi mbili dhidi ya Nigeria ugenini na timu ya taifa ya Misri utakaochezwa uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.

Mtokeo ya mechi Real Madrid vs Atletico Madrid

Friday, 16 January 2015
Posted by Unknown
Tag :

Real Madrid 2 Atletico Madrid 2
Real Madrid 2 - 2 Atletico Madrid
aggregate score: (2 - 4)
half-time: (1 - 1)
1' 0 - 1 Fernando T...
20' Sergio Ramos 1 - 1
28' Raul Garcia
46' 1 - 2 Fernando T...
49' Tiago
53' Diego Godin
54' Cristiano R... 2 - 2
56' Sergio Ramos
83' Marcelo
85' Koke
86' Daniel Carv...

Ripoti nzima ya mchezo wa Yanga vs Azam FC hii hapa

Sunday, 14 September 2014
Posted by Unknown
Tag :



IMG_7230.JPG

Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Brazil Geilson Santos “Jaja” leo amewaonyesha wapenzi wa soka nchini nini kazi yake uwanjani baada ya kuisadia Young Africans kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 huku yeye akikwamisha mabao mawili safi mchezo uliofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa jijni Dar es salaam.
Young Africans ambayo ilikua ikicheza mchezo wa Ngao ya Jamii mbele ya mashabiki wake zaidi ya elfu thelathini waliofurika kuwapa morali wachezaji, walitulia na kucheza soka tangu mwanzo wa mchezo mpaka mwisho.
Kocha Mbrazil alianza na mfumo wa 4-5-1 walinzi Juma Abdul Oscar Joshua, Kelvin Yondani na Nadri Haroub “Canavvaro”, mbele yao wakicheza viungo wa Ulinzi Mbuyu Twite na Said Juma “Makapu” wakisaidiwa na Haruna Niyonzima, Mrisho Ngasa na mbrazil Jaja akianza mshambuliaji peke yake.
Kipindi cha kwanza kilianza kwa kasi kwa timu zote kusaka bao la mapema, mipira mirefu ya Mbuyu Twite kwa Mrisho Ngasa haikuwa na madhara sana langoni mwa timu ya Azam katika dakika 10 za mwanzo.
Kiungo Said Juma “Makapu” alikosa nafasi ya kuipatia Young Africans bao la kwanza dakika ya 10 baada ya mpira wa kona uliopigwa na Niyonzima, huku Nizar Khalfani pia akikosa kuifungia pia timu yake bao baada ya shuti la faulo alilopiga kutoka mita chache pembeni mwa lango la Azam.
Young Africans iliendelea kulishambulia lango la Azam FC kupitia kwa washambuliaji wake Geilson Santos “Jaja” Mrisho Ngasa na Nizar Khalfani lakini kutoku makini kulipelekea timu zote kwenda mapumziko zikiwa sare ya kutofungana.
Kipindi cha pili Young Africans ilianza kwa kufanya mabadiliko ambapo kocha aliwaingiza Hassan Dilunga na Saimon Msuva waliochukua nafasi za Said Juma na Nizar Khalfani hali iliyopelekea kikosi cha mbrazil Maximo kutawala eneo la kiungo.
Dakika ya 58 Geilson Santos “Jaja” aliwainua vitini mashabiki, wapenzi na wanachama wa klabu ya Young Africans baada ya kuipatia timu yake bao la kwanza katikati ya walinzi wawili wa Azam FC akiitumia vizuri pasi ya Saimon Msuva.
Geilson Santos “Jaja” dakika ya 66 ya mchezo aliwainua tena vitini washabiki, wapenzi na wanachama baada ya kufunga bao la pili kwa ufundi wa hali juu, baada ya kupenyezewa pasi nzuri na kiungo Hassan Dilunga na Jaja kuukota kwa hatua moja na kisha kumchambua mlinda mlango wa Azam FC Mwandini Ali kwa kuunyanyua kwa ufundi na kuamsha shangwe na nderemo uwanjani.
Huku wapenzi wa soka wakidhania mpira umemalizika, Saimon Msuva alimaliza ndoto za timu ya timu ya Azam kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kuipatia timu yake bao la tatu na ushindi na kuifanya Young Africans kuchukua Ngao ya Jamii kwa mara ya nne tangu kuanzishwa kwake huku Simba wakiwa wamechukua mara mbili na Mtibwa Sugar mara moja.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 3 – 0 Azam FC.
Mara baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Young Africans mbrazili Marcio Maximo amesema anawashukuru wachezaji wake kwa kucheza kwa kufuata maelekezo yake hali iliyoplekea kucheza soka safi la kuburudisha linaloambatana na ushindi.
Aidha Maximo amesema baada ya ushindi wa leo maandaliz ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar yataanza siku ya jumanne ambapo kwa kesho ametoa mapumziko kwa wachezaji wote pamoja na benchi la Ufundi.
Mwisho Maximo amewapongeza vingozi, waachezaji na washabik wa Young Africans kwa sapoti wanayoitoa kwa timu na kuomba wajitokeze kwa wingi pia mjin Morogoro mwishoni mwa wiki katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.
Young Africans: 1. Deo Munish “Dida”, 2. Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4. Nadir Haroub “Cananavao” (C), 5.Kelvin Yondani, 6.Mbuyu Twite, 7.Said Juma “Makapu”/Hassan Dilunga, 8.Haruna Niyonzima/Hamis Kizza, 9.Geilson Santos “Jaja”/Hussein Javu, 10.Mrisho Ngasa/Omega Seme, 11.Nizar Khalfani/Saimon Msuva/
Azam FC: 1.Mwadini Ali, 2.Shomari Kapombe, 3.Erasto Nyoni/Gadiel Michael, 4.David Mwantika, 5.Agrrey Morrsi, 6.Kipre Balou, 7.Himid Mao/Kelvin Friday, 8.Salum Abubakar, 9.Didier Kavumbag, 10.Kipre Tchetche/Ismail Diara, 11.Leonel st.Pres/Khamis Mcha
Source: Yanga official website


IMG_6950.JPG
 
Usiku wa jana klabu ya Manchester United ilikamilisha usajili wa mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia, Radamel Falcao kwa mkopo.
Falcao ambaye alikuwa akiwindwa na vilabu vya Arsenal na Man City amejiunga na Man U akitokea klabu ya Monaco ambayo alijiunga nayo akitokea Atletico Madrid.
Usajili wa mchezaji umezungumzia na watu wengi mmoja wao ni mchezaji bora wa ulaya na dunia – Cristiano Ronaldo.
Akiongea jijini Madrid Ronaldo alisema: ‘Falcao ni mchezaji mzuri sana, nadhani Manchester United wamefanya jambo zuri kumsajili. Sidhani kabisa kama ni mchezaji asiyewafaa, ni mchezaji wa daraja la dunia na hivyo naamini huu usajili mzuri.”

Matokeo ya Chelsea vs Everton yapo hapa

Saturday, 30 August 2014
Posted by Unknown
Tag :
IMG_6886.JPG

Mechi ya mwisho ya Premier League leo hii ilikuwa kati ya vijana wa Jose Mourinho Chelsea dhidi ya vijana wa Roberto Martinez Everton.
Mchezo huo wa kuvutia uliopigwa kwenye dimba la Goodson Park umeisha kwa Chelsea kupata ushindi mzito na mkubwa kuliko wowote kwenye premier league msimu huu.
Magoli ya mapema ya Diego Costa na Ivanovic yaliwaweka Chelsea mbele kwa 2-1 mpaka timu zilipoenda mapumziko – Kevin Mirallas aliifungia Everton goli la kwanza dakika chache kabla ya kipindi cha kwanza kuisha.
Kipindi cha pili Everton walirudi kwa kasi wakijaribu kusawazisha lakini kwenyw dakika ya 67, Coleman akajifunga na kuiongezea Chelsea uongozi, lakini Naismith akapunguza pengo dakika 2 baadae, kabla ya Nemanja Matic kuongeza goli la 4 kwa Chelsea.
Samuel Eto’o akicheza mechi yake ya kwanza akiwa na Everton akafunga bao la 3 dk 76, lakini dakika 2 baadae Ramirez akapiga mkwaju wa 5 na Diego Costa kwa mara nyingine tena akafunga mahesabu kwa Chelsea kwa kufunga goli la 6 kwenye dakika 90.
Hadi mwisho wa mchezo matokeo yalikuwa yakisomeka 6-3.


Wenger: Messi made Alexis suffer at Barcelona
NA BARAKA MPEJA
ASERNE Wenger anaamini Alexis Sanchez aliathirika kama anavyoathirika Neymar wakati akiwa Barcelona kutokana na uwepo wa Lionel Messi.
Asernal ilitumia Euro milioni 40 kumsajili nyota huyo wa kimataifa wa Chile majira haya ya kiangazi na leo hii anatarajia kucheza mechi yake ya kwanza ya maandalizi ya msimu mpya.
Licha ya kucheza kama winga akiwa Barca, Alexis atachezeshwa kama mshambuliaji Emirates na Wenger anaamini atang`ara zaidi katika nafasi hiyo kutokana na kutokuwepo kwa ‘mchawi’ wake Messi.
“Kwa mara ya kwanza alitinga katika rada zangu alipokuwa Udinese na baadaye Barcelona”. Alisema Mfaransa huyo alipozungumza na The Dail Mirror.
“Ni mshambuliaji. Ni mmaliziaji mzuri ambaye alikuwa na kiwango kizuri Italia. Nilimuona pale na alikuwa amesimama vizuri. Lakini mambo yalikuwa magumu alipoenda Barcelona kama ilivyo kwa Neymar sahizi”.

“Unapomuona Neymar wa Brazil na Neymar wa Barcelona sio mtu mmoja. Naamini kuwa Alexis anaweza kucheza kushoto, kulia na mbele na ndio maana nilimfuata”.
Welcome to My Blog

Popular Post

Blogger templates

About views Blogger

Mrembo wetu wa leo

KONA YA KIJANJA YA KUJIDA VIA SNAPS

Powered by Blogger.

MY HOT BROGGER TZ

Like My Facebook Page

FOLLOW ME ON TWITTER

Contact Form

Name

Email *

Message *

- Copyright © TIMOKUCHAZ -Robotic Notes- Powered by Blogger - Designed by Johanes Djogan -