Miezi kadhaa baada ya mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda kupiga marufuku biashara ya Shisha kwenye sehemu za starehe, ulipita muda na agizo hilo likaonekana kutekelezwa japokuwa haikuchukua muda sana biashara hiyo ikarejea tena.
November 16, 2016 wakati wa uzinduzi wa mitambo ya ufuaji umeme jijini Dar es salaam, Paul Makonda alizungumzia biashara hiyo kurejea kinyemela ikiwa ni pamoja na baadhi ya wafanyabiashara kumfata na kutaka kumuhonga shilingi milioni tano ili wapewe kibali cha kuendelea na biashara hyo.
Makonda amesema kurejea kwa biashara hiyo kunampa mashaka kwamba huenda baadhi ya askari wa jeshi la polisi wamepokea hizo pesa ndiomana wanashindwa kuzuia uuzwaji wa shisha.
Kauli ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Paul Makonda imefanya Jeshi la Polisi kupitia kwa Kamanda Simon Sirro kutolea majibu kuhusu biashara ya Shisha inayofanyika pamoja na kupigwa marufuku.
“Watu wengi wameshakamatwa pale Oysterbay na majalada yanaandaliwa na mengine yameshapelekwa kwa mawakili wa serikali. Sisi tunaendelea na oparesheni kama kawaida ya kukamata wauzaji, watengenezaji na wavutaji wa shisha” – Kamanda Sirro
Unaweza kutazama video hii kupata majibu ya jeshi la polisi.