Posted by : Unknown Saturday, 30 August 2014

IMG_6886.JPG

Mechi ya mwisho ya Premier League leo hii ilikuwa kati ya vijana wa Jose Mourinho Chelsea dhidi ya vijana wa Roberto Martinez Everton.
Mchezo huo wa kuvutia uliopigwa kwenye dimba la Goodson Park umeisha kwa Chelsea kupata ushindi mzito na mkubwa kuliko wowote kwenye premier league msimu huu.
Magoli ya mapema ya Diego Costa na Ivanovic yaliwaweka Chelsea mbele kwa 2-1 mpaka timu zilipoenda mapumziko – Kevin Mirallas aliifungia Everton goli la kwanza dakika chache kabla ya kipindi cha kwanza kuisha.
Kipindi cha pili Everton walirudi kwa kasi wakijaribu kusawazisha lakini kwenyw dakika ya 67, Coleman akajifunga na kuiongezea Chelsea uongozi, lakini Naismith akapunguza pengo dakika 2 baadae, kabla ya Nemanja Matic kuongeza goli la 4 kwa Chelsea.
Samuel Eto’o akicheza mechi yake ya kwanza akiwa na Everton akafunga bao la 3 dk 76, lakini dakika 2 baadae Ramirez akapiga mkwaju wa 5 na Diego Costa kwa mara nyingine tena akafunga mahesabu kwa Chelsea kwa kufunga goli la 6 kwenye dakika 90.
Hadi mwisho wa mchezo matokeo yalikuwa yakisomeka 6-3.

Welcome to My Blog

Popular Post

Blogger templates

About views Blogger

Mrembo wetu wa leo

KONA YA KIJANJA YA KUJIDA VIA SNAPS

Powered by Blogger.

MY HOT BROGGER TZ

Like My Facebook Page

FOLLOW ME ON TWITTER

Contact Form

Name

Email *

Message *

- Copyright © TIMOKUCHAZ -Robotic Notes- Powered by Blogger - Designed by Johanes Djogan -