Wapenzi
ambao wapo katika uhusiano lakini hawajui mambo ya kufanya ili wawe bora kwa
wapenzi wao. Mada hii itagusia pande mbili. Upande wa kwanza ni kwa wale ambao
ndiyo kwanza wapo katika hatua za mwanzo kabisa na wapenzi wao na upande wa
pili ni kwa wale ambao tayari wapo katika uhusiano lakini hawajui jinsi ya
kuwafanya wawe bora kwa wapenzi wao.
Inawezekana
wewe ukawa mmoja wao, sasa huna sababu ya kukata tamaa na kuona kuwa huna
thamani tena kwa mpenzi wako. Kwa kufuatilia vyema vipengele 10 vifuatavyo,
nina imani utakuwa mpya na penzi lako litazidi kudumu zaidi na zaidi.
1. MWANZO
WA PENZI
Siku zote
nimekuwa nikisisitiza kuwa, jinsi unavyoanza ndivyo utakavyomaliza! Kama
ulianza vibaya uhusiano wako tegemea kumaliza vibaya, lakini kama
Kama
unatarajia kuingia katika uhusiano na mpenzi mpya hakikisha hujionyeshi tofauti
na hali yako halisi ilivyo! Jifunze kujikubali, hata kama unafanya kazi ambayo
unadhani ni hadhi ya chini, mbainishe mpenzi wako hali halisi ilivyo. Kama
anakupenda, kazi yako haiwezi kupunguza mapenzi baina yenu.
Ikiwa
ndiyo kwanza mnaanza uhusiano, zingatia hili, na kama mpo katika uhsiano kwa
muda mrefu ukagundua wazi kuwa kuna mahali ulikosea, anza kufanya mabadiliko
kuanzia sasa. Bado hujachelewa, mwambie ukweli naye atakuheshimu kutokana na
ukweli wako.
Kudanganya
hakuna mantiki, kudanganya ni utumwa, usikubali kuingia katika utumwa au
kifungo cha aina hiyo. Ukweli ni silaha ya kwanza katika mapenzi, anza hivyo
kuanzia mwanzo na kama ulikosea, ulijisahau au hukujua, basi anza leo!
2.
USIJICHUKIE
Itakuwa
kichekesho kama utasema unampenda mpenzi wako wakati wewe mwenyewe hujipendi!
Huwezi ukasema unamthamini mpenzi wako wakati thamani yako mwenyewe huitambui.
Naamini
tunakwenda sawa, kama unashindwa hata kuoga na kubadilisha nguo safi nani
atakayekupenda? Huwezi kuwa wa kisasa kama huzingatii usafi, hakuna
atakayevutiwa na wewe kama wewe hutaki kujivutisha. Sio ajabu mpenzi wako
akakutosa kwa sababu tu huna muonekanano mzuri kwa rafiki zake.
Nani
atakayekupenda wakati wewe mwenyewe huonyeshi kama unajitambua?
Jikubali,
jithamini! Kuwa msafi wakati wote, kauli zako ziwe safi siku zote mpenzi wako
atakuwa huru kuwa na wewe. Isifikie hatua mpenzi wako akataka kutoka na wewe
lakini akasita kwasababu hajui ukija utakuwa umevaa nguo za namna gani. Upo
hapo?
3. MWONEKANO
WAKO
Mwonekano
wako unaweza kukuanisha jinsi ulivyo kwa wanaokutazama, wakati mwingine
inawezekana ukatafsirika tofauti na ulivyo kutokana na jinsi unavyovaa na tabia
zako zingine!
Lazima uwe
kijana wa kisasa, kwa kuzingatia hilo unapaswa kuwa makini kwa kila kitu
kinachoonekana kwa wanaokutazama. Jenga mazoea ya kutambua aina ya nguo na
mahali ulipo, usivae nguo za ufukweni ofisini au nguo za mtaani ukavaa ofisini!
Wanaokuangalia
wanapata taswira ya jinsi usivyo makini au makini kutokana na mavazi yako. Vaa
nguo safi kila wakati, labda kama unafanya kazi ambayo inakulazimu kuwa mchafu,
ila baada ya hapo unapaswa kuwa msafi. Ukizingatia hili utamfanya mpenzi wako
afurahie kuwa na wewe siku zote. Amini popote ulipo, jinsi ulivyo ndivyo
anavyoonekana mpenzi wako.
Post a Comment