Ili
uwe na kucha maridadi zinahitaji usafi
kawaida kucha zilizo safi ndizo hasa zinazokubali
polishi
Ni
vyema kutambua kwamba wakati wa kupaka rangi tumia mipako michache kwa
kila mpako na kila mpako uachie ukauke kabla ya kuanza mpako mwingine.Na ile ya mwisho inatakiwa kuwa bomba zaidi kwa kuwa ndio hasa itakayokuwa inatunza matabaka mengine yote.Utengenezaji
mzuri wa kucha si lazima uwe wa kwenda katika mapumziko au kuonyesha
mtu ni kitu ambacho kinafaa kufanywa ili uwe mrembo. Unaweza
kujipaka rangi mwenyewe au kuwambia mtu akupake rangi.Kuna hatua kadhaa
ambazo unatakiwa kuzifanya kabla ya kupaka rangi kucha zako.
Hatua ya kwanza ni........
1) kuondoa rangi zote za awali.kwa kufanya hivyo rangi mpya itakuwa ina uwezo wa kushika katika kucha.Pia kunasaidia rangi yako mpya isitibuliwe na rangi ya zamani kwa namna yoyote ile.Unaweza
kuondoa rangi ya zamani kwa kutumia Nail polish remover.
2) Tumia msasa mgumu kuzisawazisha kucha zako baada ya hapo pitisha msasa laini kuzifanya kucha zako ziwe soft nyunyizia maji kidogo halafu futa na taulo hapo ndio unaweza kupaka kararesi
3)Karalesi inayofaa kuanza ni Base Coat
Anza kupaka katikati kwa kuanzia nyuma kupeleka
mbele kisha nenda pembeni na pembeni.Na baada ya kukauka unaweza
kupaka rangi yako yoyote
4)Kisha paka ile ya mwisho
ambayo ndiyo italinda rangi yenyewe yaani top coat . top coat husaidia
sana kuweka rangi kwa muda mrefu. Top coat ni polishi isiyokuwa na rangi
5)na kama unataka kuweka stika iweke mapema kabla ya kuweka top coat.rangi nzuri na zilizotulia zinakufanya uweMrembo zaida
Asante by Timokuchaz
Post a Comment