Moja ya headlines zinazomuhusu mwimbaji sataa wa Bongofleva kutoka kundi la Yamoto Band, Beka Flavour leo July 20, 2017 ni kuhusu kushikiliwa kwake na Jeshi la Polisi DSM kwa mahojiano yaliyodumu kwa saa Tisa kuanzia saa tano Asubuhi hadi saa mbili Usiku.
Ayo TV na millardayo.com zimempata Beka Flavour>>>”Nipo hapa tangu saa tano Asubuhi kwamba natuhumiwa kutapeli pesa za jamaa mmoja kupitia mitandao yangu ya kijamii. Huyu jamaa anaishi Kigoma na anadai kuwa alikuwa akizungumza na mimi na anasema hakuwahi kuonana na huyo Beka basi nilipata taarifa a kuripoti katika kituo hiki na niliporudi kutoka Safari ndio nimelifika hapa.
“Nimetoka kwa dhamana na kikubwa ningependa kuwaomba watu na mashabiki wengi kwamba watu wanaotumia majina yetu sio kitu kizuri kwani kama huyo wa Kigoma aliyetuma pesa anadai ametuma zaidi ya milioni 8. Kwa hiyo, wawe makini na mitandao feki kwani Maromboso, Enoki na wengine hatuna kurasa za Facebook.” – Beka Flavour.
“Kwa sasa nina Manager mpya mbali na Yamoto Band” – Becka Flavour…PLAY kwenye hii VIDEO kutazama kila kitu!!!
Post a Comment