Posted by : Unknown Tuesday, 22 July 2014



https://www.facebook.com/Timokuchaz

Kufuatia sakata la Flora Mbasha na mumewe likumuhusisha moja moja kiongozi wa kiroho Mchungaji Gwajima, habari tulizozipata ni kwamba mchungaji huyo amekimbia nchi….

Habari toka chanzo cha kuaminika kilichopo ndani ya kanisa la mchungaji huyo ni kuwa Gwajima hivi sasa ameshauza karibia robo tatu ya mali zake na kwamba moja kati ya magari yake ya kifahari huenda likanunuliwa na mwanamuziki Diamond.

“Jamaa hivi tunavyoongea anaweza akawa ameshatoroka tayari, maana hili sakata limeanza kumwendea hovyo na wiki iliyopita kuna madalali walikuja hapa wakiitaka gari yake aina ya Hammer, wakidai kuwa inataka kununuliwa na mwanamuziki Diamond,” kilisema chanzo cha habari hii.

Kikaendelea kumwaga data kuwa karibu wiki zima lililopita mchungaji huyo alikuwa kwenye mipango ya kuuza baadhi ya nyumba zake na kwamba hata familia yake hivi sasa haiko kwenye makazi yake anayoishi siku zote…

“Hata familia yake sijaiona karibu wiki mbili hapa kanisani na taarifa tulizonazo karibu waumini wengi tu ni kwamba jamaa anataka kuhama nchi lakini hatujui ni nchi gani anayotaka kwenda kufanya makazi yake tena ya kudumu,” alisema.

Habari hizo zinadai kuwa baadhi ya waumini wamepanga kugawana mali kadhaa za kanisa pamoja na za Gwajima mwenyewe endapo itagundukia kuwa ametoroka kweli….

“Kuna baadhi ya waumini wamekerwa sana na hii skendo ya Flora Mbasha, wamekuwa wakijiapiza kwamba hata zile mali zake ni halali yao kwani zinatokana na sadaka wanazotoa kila siku, inasikitisha sana kwa kweli.” alisema mtoa habai hii.

Inasemekana kuwa mchungaji Gwajima amepanga kuwaaga waumini wake kama vile anakwenda kueneza neno katika mataifa mengine, lakini ukweli ni kwamba anataka kuondoka ili kukwepa aibu kutokana na mambo yanayoendelea…

“Jamaa yupo kwenye hali ngumu, hii ishu ya Flora Mbasha imemuweka katika wakati mgumu sana kwa sababu amekuwa akinyooshewa vidole sana, na kuna baadhi ya wazee wamekuwa wakimtaka atoe tamko rasmi ili kukwepa hiki kikombe cha aibu,” kilisema chanzo hicho.

Mwandishi alimpigia simu Gwajima lakini simu yake haikupatikana, na hata Diamond naye alipopigiwa simu ili kujua kama kweli anataka kununua gari la Gwajima, simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi hakujibu kitu.

KAMA ULIKUWA HUJAJIUNGA NASI

Welcome to My Blog

Popular Post

Blogger templates

About views Blogger

Mrembo wetu wa leo

KONA YA KIJANJA YA KUJIDA VIA SNAPS

Powered by Blogger.

MY HOT BROGGER TZ

Like My Facebook Page

FOLLOW ME ON TWITTER

Contact Form

Name

Email *

Message *

- Copyright © TIMOKUCHAZ -Robotic Notes- Powered by Blogger - Designed by Johanes Djogan -