Mashuhuda wa tukio hilo wamesema ndege hiyo imepata ajali hiyo muda mfupi uliopita ambapo iligonga jengo hilo na kuwaacha takribani watu kumi wakiwa wamenasa ndani ya jengo na haijafahamika bado kuhusiana na hali zao.
Hakuna taarifa zinazoelezea kuhusiana na ukubwa wa ndege hiyo wala idadi ya watu waliokuwamo ndani. Picha zilizoenea mitandaoni zinaonyesha moto mkubwa unaowaka uwanjani hapo.
Post a Comment