Posted by : Unknown
Thursday, 23 October 2014
Sote tumeusubiri kwa hamu na sasa wimbo
mpya kabisa wa Mwana FA na Alikiba umewasili rasmi. Baada ya Mwana FA
kutoa wimbo wa Mfalme live katika tuzo za KTMA 2014 msanii huyu
ameungana na mfalme wa bongo flava yaani Alikiba ili kuwaletea mashabiki
wake kazi nyingine kali. Producer wa
wimbo huu si mwingine bali ni
Marco Chali wa kutoka MJ Records ya jijini Dar Es Salaam. Katika
kuurekodi wimbo huu kumekuwa na matoleo manne tofauti ambayo wadau
walikuwa wakisindwa kuamua ni upi wa kuachia kwa kuwa zote zimesimamia
kucha. Mwana FA na kampuni ya LifeLine
ambaye yeye pia ni mkurugenzi
wameamua kuuachia wimbo huu moja kwa moja kupitia Mkito.com ili
kuhakikisha unawafikia wapenzi wake wengi zaidi na kuhakikisha kuwa kuna
maslahi yanapatikana katika kazi hii. Pakua wimbo huu mpya kabisa sasa
upate flava kali.
Related Posts :
- Back to Home »
- MUSIC »
- NEW AUDIO: Mwana FA (@MwanaFA) ft. Ali Kiba (@OfficialAliKiba) – KIBOKO YANGU
