October
9 2014 nchi ya Uganda iliazimisha uhuru wake huku rais wake Yower
Museven akizungumza mambo muhimu matatu kwa wananchi wake ambapo ishu ya
kwanza ni kuwataka wananchi wake kuwa makini kutokana na tishio la
magonjwa ya Marburg pamoja na Ebola hivyo waache kusalimiana kwa
kushikana mikono pamoja na kukumbatiana bila kuwepo ulazima wa kufanya
hivyo.
Alisema magonjwa hayo kwa sasa yameonekana kuchukua nafasi kubwa
duniani na amewataka kuwa makini zaidi ili yasizidi kusambaa lakini pia
kumekuwa na utamaduni wa baadhi ya watu hasa wanaoishi maeneo yenye
misitu kula nyama za nyani ambazo magonjwa hayo yanaaminika kuanzia
huko, nao pia amewataka waache ili haya magonjwa ya ajabu yasije kwa
binadamu.
Kitu kingine ambacho rais huyo alizungumza ni kitendo cha mabosi wa
mahakama ya The Hague ya Uholanzi kumtaka rais mwenzake wa Kenya, Uhuru
Kenyatta kuhudhuria kikao cha kujibu tuhuma dhidi yake kuhusiana na
ghasia zilizotokea nchini kwake na kusema kililenga kudharau na
kusitisha mkutano uliofanyika juzi nchini kwake.
Alisema pamoja na Serikali ya nchi hiyo kuomba rais Kenyatta
kuhudhuria mkutano huo muhimu lakini mahakama hiyo ilionekana kukataa na
kulazimisha ahudhurie katika kesi hiyo.
Hata hivyo Kenyatta alikanusha tuhuma za yeye kuhusika na ghasia
zilizosababisha kupoteza maisha ya zaidi ya watu 1200 huku wengine zaidi
ya laki sita wakikosa mahali pa kukaa mara baada ya kumalizika kwa
uchaguzi mkuu na jambo la mwisho alilozungumzia ni kuhusu timu ya Taifa
ilo ambalo inakabiliwa na mchezo dhidi ya Togo ambapo aliwatakia kila la
Kheri.