SHERIA YA MAKOSA YA MITANDAO TAYARI
IMESAINIWA NA RAIS.
Rais Jakaya Kikwete tayari ameshasaini sheria yenye utata ya
makosa ya mtandao na muda wowote kuanzia sasa itaanza
kutumika rasmi
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Profesa
Makame Mnyaa Mbarawa, amesema hayo leo wakati
akizungumzia masuala mbali mbali yanayohusu sheria hiyo
ambayo kupitishwa kwake kumesababisha malalamiko mengi
kutoka kwa wadau kuwa itaminya uhuru wa habari, kuingilia
faragha pamoja na uhuru wa watu kuwasiliana.
Ufuatao hapa chini ni uchambuzi kidogo kuhusu baadhi ya
vipengele vilivyozua utata katika muswada huu uliokuwa
umetolewa
1. Kifungu 7 (2b): Mpokeaji wa ujumbe (receiver) anaweza
kushtakiwa kwa kosa la kupokea ujumbe ambao sheria
imeufanya kuwa wa jinai. (Mfano: Mtu akikuforwadia ujumbe,
ukiupokea na wewe umefanya kosa la jinai). Vs East Africa Television (EATV) Habari
2. Kifungu 8: Itakuwa ni kosa la jinai kama mtu ataweka wazi
nyaraka za siri za serikali hata kama ni nyaraka ya kusaidia
nchi kwa ujumla (Mfano: Matumizi mabaya ya mali ya
umma).
3. Kifungu 14: Picha yoyote yenye mwelekeo unaoweza
kuonekana kama ‘mchafu kingono’ inaweza kupelekea mtu
kufungwa hadi miaka 10 au kulipa milioni 30; (Mfano: mtu
kaposti picha yake ambayo sio ya ponografia lakini
‘ikatafsiriwa’ hivyo. Sheria haijatafsiri ponografia!)
4. Kifungu 23: Je, ulijua kuwa ‘kusababisha maudhi ya hisia’
kwa mtu mwingine ni unyanyasaji na unaweza kufungwa
kifungo kisichopungua mwaka mmoja?
5 Kifungu 22: Ukiweka ujumbe katika mtandao na ukaufuta au
kuuboresha, kama ukishtakiwa kwa kuweka ujumbe huo
unaweza kuhukumiwa pia kwa adhabu ya kuuboresha au
kuufuta. (Mfano: unapofuta ‘status’ zako za WhatsApp,
unaweza shitakiwa kwa kuchelewesha ushahidi kisa tu ulifuta
na hamna mtu anayeweza kujua ulifuta kwa kusudi au la.)
6. Mkuu wa kituo cha Polisi chochote kile nchini anaweza
kuagiza wewe umpatie simu/laptop yako au taarifa zako zote
(kwenye email, chats) au hata vifaa vyako au ofisi yako kwa
ajili ya upelelezi bila oda ya Mahakama.
7. Serikali kupitia waziri husika ndio ina mamlaka ya kusema
jambo lililowekwa kwenye mtandao ni la kweli, uongo au la
kupotosha
Post a Comment