Ukiona umemtumia mpenzi wako/mchumba wako/mchepuko wako/mke wako au hata
rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaida tu kwaajili ya kumsalimia
lakini yeye akakujibu moja kati ya majibu yafuatayo, tafadhali sana
usiendelee kuchat nae maana kinachofuata hapo ni majanga tu.
KWA MFANO:
1. Ukimtumia sms ''Mambo mpenzi wangu?'' akikujibu ''mambo mabaya'',
usimuulize kwanini mambo mabaya, ukimuuliza atakwambia kuwa ''sina hela
dear''
2. Ukimtumia sms ''Maisha yanasemaje kipenzi changu'' akikujibu ''maisha
magumu hubby wangu we acha tu'' usimuulize kwanini, ukimuuliza kwanini
atakwambia ''nimefulia mwenzio kama nini sijui''
3. Ukimtumia sms ''Mbona kimya sana mchumba wangu, umenitupa kiasi
hicho'' akikujibu ''sijakutupa wangu yaani mambo hata hayaendi''
usimuulize kwanini mambo hayaendi, ukimuuliza atakwambia kuwa ''yaani
sina kitu mpenzi wangu, simu ilikuwa haina hata hela ya kubeep''
4. Au ukiona mwanamke anaanza kwa kukwambia nikwambie kitu? We mkatalie
kiutani utani tu, mwambie usiniambie, hata akikomaa vipi akwambie
mwambie sitaki uniambie huku unafanya kama utani lakini moyoni unakuwa
upo serious.
Ni mara chache sana mwanamke akikwambia kuwa mambo mabaya, maisha magumu
au mambo hayaendi huwa na matatizo mengine kama kuumwa, misiba.... n.k
lakini THE REST ni wapigaji mizinga tu. Akikwambia maisha magumu mjibu
''pole wangu, mambo mengine vipi?''
Ukipewa majibu kama hayo, chagua moja, either usiendelee kuchat nae
mpaka badae kidogo au mbadilishie maada ili kukwepa huo mzinga ambao
unakuja mbele yako.