Showing posts with label MICHEZO. Show all posts
Ushindi mwingine wa KRC Genk ya Samatta Europa League leo July 28 2016
Thursday, 28 July 2016
Posted by Unknown
Tag :
MICHEZO

Usiku wa July 28 klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji inayochezewa na nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars Mbwana Samatta ilishuka tena dimbani kucheza mchezo wake wa kwanza wa round ya pili wa kuwania kucheza hatua ya makndi ya Kombe la UEFA Europa League dhidi ya Cork City ya Ireland.
Mchezo wa kwanza wa round ya pili ya Europa League KRC Genk wameanzia katika uwanja wao wa nyumbani wa Cristal Arena
wenye uwezo wa kuchukua mashabiki zaidi ya 24000 na kufanikiwa kuibuka
na ushindi wa goli 1-0, goli ambalo lilifungwa na mjamaica Leon Bailey dakika ya 31 baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa mshambuliaji wa Kigiriki Nicolaos Karelis.

Hata hivyo licha ya KRC Genk kupata ushindi huo wakiwa pamoja na nyota wao kutoka Tanzania Mbwana Samatta, bado wana wakati mgumu katika mchezo wa marudiano watakaocheza August 4 Ireland, kwani watakuwa wanahitaji ushindi au sare ya aina yoyote ile ili waweze kusonga mbele katika hatua inayofuata na kuitoa Cork City.
Kama utakuwa unakumbuka vizuri KRC Genk wamekutana na Cork City, baada ya kuitoa Buducnost ya Montenegro kwa mikwaju ya penati 4-2, baada ya mechi yao ya mwisho kumalizika kwa Buducnost
kuibuka na ushindi wa goli 2-0 ila kutokana na kuwa na aggregate ya 2-2
walilazimika kucheza dakika 120 na baadae mchezo ukaamuliwa kwa mikwaju
ya penati.
VIDEO: Messi kasherehekea Birthday yake leo June 24, mambo matano ya kufahamu
Saturday, 25 June 2016
Posted by Unknown
Tag :
MICHEZO
June 24 Lionel Messi anakumbuka siku yake ya kuzaliwa, leo June 24 2016 anatimiza umri wa miaka 29, Lionel Messi ameweka rekodi nyingi katika soka ikiwemo ya kutwaa Ballon d’Or mara 5. Mtu wangu wa nguvu naomba nikusogezee mambo matano kuhusu Lionel Messi leo katika kumbukumbu yake ya kuzaliwa.
1- Mechi amecheza juml ya mechi 643.
2- Amefanikiwa kufunga jumla ya magoli 508.
3- Ametoa assist 213.
4- Ameshinda jumla ya mataji 28 katika soka.
5- Lionel Messi amefunga zaidi ya hat-trick 30 katika soka.
GOAL AND HIGHLIGHTS: MO BEJAIA VS YANGA JUNE 20 2016, FULL TIME 1-0
Samatta Aitungua Chad Na kuonyesha kweli yeye ni wa kimataifa na kuweka rekodi ya Tanzania kwa Taifa la Chad
Thursday, 24 March 2016
Posted by Unknown
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars March 23 imeshuka katika dimba la Idriss Mahamat kucheza na wenyeji wao timu ya taifa ya Chad katika muendelezo wa michezo ya makundi ya kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON) itakayochezwa mwaka 2017.
Huu ulikuwa ndio mchezo wa kwanza wa Mbwana Samatta akiichezea Taifa Stars kama nahodha wa timu hiyo, katika mchezo huo uliochezwa Chad, Taifa Stars imeibuka na ushindi wa goli 1-0, goli la Taifa Stars lilifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 30, baada ya kutumia vyema krosi ya Farid Musa.
Samatta amefanikiwa kuitunzia Tanzania rekodi dhidi ya Chad, kwani mara ya mwisho Taifa Stars alikutana na Chad, ugenini na kufanikiwa kuibuka kwa ushindi wa goli 2-1. Magoli ya Taifa Stars wakati huo yalifungwa na Mrisho Ngassa dakika ya 11 na Nurdin Bakari dakika ya 88, huku goli la Chad la kufutia machozi lilifungwa na Mahamat Labbo dakika ya 12.
Msimamo wa Kundi G ulivyo hadi sasa
Taifa Stars itarudiana na Chad Jumatatu ya March 28 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, huku ikiwa imebakiza mechi mbili dhidi ya Nigeria ugenini na timu ya taifa ya Misri utakaochezwa uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.