Rapper mdogo kuliko wote Tanzania "Dogo D" mwenye umeri chini ya miaka
15 kutoka Mwanza ameachia wimbo unaowadiss wasanii kibao wakubwa wasanii
wa mwanza Mo Music na Yong Killer lakini pia hakuwaacha wasanii wengine
kama Nay wa Mitego, Dogo Janja, Pnc na wengineo
Ngoma hiyo aliyoipa jina la "Wamenichokoza" akiwa amemshirikisha King Silver amemdiss Mo Music na Nay wa Mitego kwa kusema
"mwanzoni ulipokwenda pamoja tulikwenda kuhit basi nenda, kufanya ngoma yangu ndio unanipiga kalenda
wamitego acha poz kama dem, kama kidume kweli kwanini hupokei simu.
hakuishia hapo aliendelea na kumdiss Young Killer na Dogo Janja kwa kusema
"Hakuna baba mwenye gari kuna baba mwenye nyumba, msodoki acha uongo
kusema umejenge nyumba"....Dogo janjaro chunga utapauka utadhani goti la
mbuzi wakati kwa madee unakula na kunywa nkujamba tu ushuzi"
alipofikia kumdiss msanii Kimbunga Dogo D alisema
"kimbunga mchawi jipange kuroga kwangu, wachawi wenzako wamekuwa wake
zangu.....", Kala pina kabuma hajui afanye nini, waambie waeusi navaa
miwani na bado naona gere
sikiliza wimbo wote hapa chini na alichokisema young killer na dogo d mwenyewe
Nilipata nafasi ya kuongea na Dogo D mwenyewe na hiki ndicho alichokisema
"Unajua mziki ni changamoto halafu mi pia nipo nao peace wote, Nay nipo
nae peace, young killer na Mo Music wote nipo nao peace, halafu pia
ngoma hiyo "wamenichokoza" imeongelea ukweli mtupu, maana Nay pia
nikimpigiaga simu sometime hapokei, unajua Mo Music kipindi haijahit
basi nenda tulikuwa nae peace ila ilivyohit basi nenda akabadilika so
hii ngoma imeongelea ukweli asilimia kubwa sana na ndio maana ngoma hii
inapenya na inazidi kupenya na nikaamua kuwachana ambao wanazingua siku
zote"
nilipoongea na Young Killer alisema
"kwa upande wangu kidogo nimechukulia kawaida kutokana na dogo amekaa
aka create idea, ameangalia akaona idea flani ambayo inafaa kwa upande
wake kwahiyo akaamua achane, ametuchana kwa respect hajavuka mipaka
hajatudiss saaana kusema kwamba tuweze kujukua hatua labda tumpige
kwasababu yule ni mdogo na sidhani kama anaweza kukaa akafikiria
kunidiss indeep zaidi kutakana na mimi mwenyewe kuwa ni sehemu kubwa
sana ya msaada wake kwahiyo naamini ni idea na wala hakuna tatizo lolote
baina yangu mimi na yeye au hata hao wengi aliowachana.kwahiyo ni idea
ya kawaida kabisa ametudiss kwa kutonyesha kabisa, hajavuka mipaka na
nimechulia powa kwasababu mimi hata ngoma iliyotoka kabla ya hii
nimefanya nae, na hata kipindi anaifanya ngoma hii alinipigia akaniambia
nimefanya ngoma hii na hii na akanitumia na nikaisikiliza so binafsi
nilimwambia fresh tu kutokana na idea, so binafsi haijanipain na
nimeichukulia fresh tu naamini ni idea tu kila kitu kinaenda kama
kilivyopangwa yeaah"
nilipomtafuta Nay alisema hataki kuongelea hiyo ishu
Post a Comment