Posted by : Unknown
Saturday, 25 October 2014
Waziri mkuu wa Canada, Stephern Harper.
Akitoa tamko hilo waziri mkuu wa Canada 
Stephen Harper amesema shambulio hilo ‘haliitetemeshi’ Canada, bali 
linaiongezea nchi hiyo ujasiri.
Rais wa Marekani Barack Obama na waziri 
mkuu wa Uingereza David Cameron wamelaani kitendo hicho kwa kukiita ni 
cha kukiita ni cha ‘kikatili’, huku wakisisitiza kuwa wakati huu ni wa 
kuwa macho zaidi kwa kuimarisha ushirikiano baina yao katika kupambana 
na ugaidi.
Cameron ameeleza kuwa tayari kushirikiana na Canada kwa msaada wowote utakaohitajika katika kukabiliana na hali hiyo.
Taarifa kutoka shirika la utangazaji 
nchini Ufaransa RFI linasema bado askari polisi wa kikosi maalum cha 
usalama wameendelea kulizunguka eneo hilo japo hali ya usalama 
imeimarika kwa sasa.
Canada imesema waliouawa kutokana na 
shambulio hilo ambao ni mwanajeshi koplo Nathan Cirillo na aliyekuwa 
askari wa bunge Kevin Vickers wamekufa kishujaa, huku polisi wakiendelea
 kumsaka mshukiwa wa tukio hilo aliyetajwa kwa jina la Michael Zehalf- 
Bibeau.
Kevin Vicker, askari wa bunge aliyeuawa kwa kupigwa risasi katika shambulio hilo
Koplo
 Nathan Cirillo , mwanajeshi aliyeuawa kwa kufyatuliwa risasi akiwa 
analinda katika makumbusho ya vita ya dunia jirani na jengo la Bunge la 
Canada.
Kwa habari za haraka Like Facebook Page yetu   >>>>>Timokuchaz <<<<<   Ili upate vitu kibao
 
Post a Comment