Jeshi la polisi kwa kushirikiana na Jeshi la Ulinzi la
wananchi Tanzania(JWTZ) wamefanikiwa kulipua bomu lililotegwa katika eneo
la kituo cha kurushia matangazo kilichopo mshangano cha shirika la
utangazaji Tanzania (TBC) Songea Mkoani Ruvuma siku ya jana majira ya saa moja
jioni.
Bomu hili linalosadikiwa kutengenezwa kienyeji nawatu
wasiojulikana lilitegwa hatua zinazokadiliwa thelathini kutoka kitika
kituo kilipo katika eneo ambalo askari wa usalama barabarani wanakaa kwa ajili
kufanya kazi zao za kila siku.
Kamanda wa Polisi
mkoa wa Ruvuma Mihayo Msikhela amesema kwamujibu wa wataalamu wa milipuko
kutoka jeshi la Ulinmzi la wananchi wa Tanzania bomu hili linaonekakana
limetengenezwa kienyeji.
ameitaka jamii kutoa ushrikiano kwa jeshi la polisi
ili liweze kuwabaini watu waliowalipua kwa bomu lililotengenezwa kienyeji
askari polisi watatu wakiwa katika doria katika kata ya misufini
manispaa ya songea.
Msikhela amesema Jeshi la polisi linafanya jitihada za
kuwapata watu hawa wanaohusika na mtandao huu wa utegaji wa mabomu na ulipuaji,
Aidha ameitaka jamii kutoa ushrikiano kwa Jeshi la Polisi
ili liweze kuwabaini watu wanaousika na matukio ya
namana hii.
Na hii ni mara ya pili katika manispaa ya songea
kutokea kwa matukio haya ambapo tarehe Oktoba 16 mwaka huu askari
watatu wa jeshi la polisi katika wilaya ya Songea mkoani Ruvuma, walijeruhiwa
kwa kitu kinachosadikiwa kuwa ni bomu la kutupwa kwa mkono ambalo lilisadikiwa
kutengenezwa kienyeji, katika eneo la matarawe mjini songea mkoani Ruvuma.
Askari
hao walikutwa na mkasa huo saa moja na nusu usiku wakati wakiwa katika doria
ambao ni WP Felista Abel,
PC John Kaduma na PC Ramadhani Ally
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Songea Joseph Mkirikiti akizungumza na mtandao
huu wa demasho kwa njia ya simu amesikitishwa
na kitendo hicho cha utegeji wa Mabomu ikiwa nikutaka kuhatarisha amani iliyopo
katika mkoa huu wa Ruvuma.
Aidha
amesema serikali kupitia vyombo vyake vya ulinzi na usalama watahakikisha
wanawasaka na kuwakamata walewote wanaohusika na vitendo hivi.
Follow page zetu
Post a Comment