Archive for March 2016


 
 
Licha ya jitihada za serikali kutangaza vita dhidi ya wauzaji na wanunuzi wa miili ya kinadada na kuwataka waache kwa kuwa ni kinyume cha maadili na sheria ya nchi, warembo hao (sio walio pichani ukurasa wa nyumawamedaiwa kukaidi agizo hilo huku wakidai kama aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Yusuf Makamba alishindwa basi hata mkuu mpya wa mkoa huo, Paul Makonda hatawaweza.

Hivi karibuni, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro alitangaza oparesheni maalum ya kuwasaka madada poa hao, sambamba na wateja wao akidai wanakiuka sheria na maadili ya Mtanzania jambo ambalo liliungwa mkono na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu.
Mara baada ya agizo hilo la serikali kutolewa, wanahabari wetu walifanya uchunguzi katika maeneo ambayo yamezoeleka kwa biashara hiyo na kukuta baadhi yao wakiendelea kama kawaida kana kwamba hakuna agizo lolote lilitolewa.

Risasi lilipita maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar na kuwakuta akina dada hao wakiendelea na biashara hiyo kwa kujipanga barabarani kuelekea baa maarufu ya Meeda ambapo wanahabari wetu waliojifanya wateja walipowauliza kulikoni hawaogopi nguvu ya dola, walisema wao wameshindikana tangu enzi za Makamba, Kandoro na Said Meck Sadick (aliyepita) hivyo hata huyu wa sasa, Makonda hatawaweza.

Wewe hii ni nguvu ya soda. Hatuwezi kuacha unafikiri tutakula wapi? Hii kazi tumeanza kitambo, tangu enzi za Makamba aliyekuwa hatari kweli kukemea biashara hii lakini tulimshinda. Akaja Sadick naye tukamgaragaza sembuse huyu Makonda aliyepewa jiji hili juzi tu?” alisema dada poa mmoja aliyekataa kutaja jina lake.

Maeneo mengine ya Jiji la Dar ambayo Risasi lilibaini kuwa biashara hiyo bado inaendelea kama kawaida ni pamoja na Sinza-Afrikasana (maarufu kama Conner Bar), Buguruni (Kimboka Bar, Rozana), Temeke na Kinondoni-Makaburini.

Alipotafutwa Makonda kuhusiana na suala hilo alisema atalizungumza kwa kirefu baada ya Sikukuu ya Pasaka lakini mwanahabari wetu alipombana zaidi ili aweze kutoa ufafanuzi kwa kuwa madada poa hao wamekaidi agizo la serikali, aliahidi kulizungumzia siku iliyofuata (Machi 21) lakini hata hivyo siku hiyo alipopigiwa simu hakupokea.


Hata mwandishi wetu alipomtumia ujumbe mfupi wa maandishi kumsisitiza azungumzie suala hilo, Makonda hakujibu chochote.

Aidha, mwandishi wetu pia alimtafuta Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro ili aweze kuzungumzia suala hilo, aliomba atafutwe baadaye kwa kuwa alikuwa kwenye kikao. Baadaye simu yake haikupatikana hewani.

GPL


Rais John Pombe Magufuli aliwateua wakuu wapya wa mikoa Tanzania bara March 13 2016 ambapo kati yao 13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, watano wamehamishwa vituo vya kazi na mmoja amepangiwa Mkoa mpya wa Songwe sasa wakati wa kuwaapisha kuna mmoja wa viongozi aliteleza kufata kanuni za viapo, tazama kwenye hii video hapa chini.


Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars March 23 imeshuka katika dimba la Idriss Mahamat kucheza na wenyeji wao timu ya taifa ya Chad katika muendelezo wa michezo ya makundi ya kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika  (AFCON) itakayochezwa mwaka 2017.

Huu ulikuwa ndio mchezo wa kwanza wa Mbwana Samatta akiichezea Taifa Stars kama nahodha wa timu hiyo, katika mchezo huo uliochezwa Chad, Taifa Stars imeibuka na ushindi wa goli 1-0, goli la Taifa Stars lilifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 30, baada ya kutumia vyema krosi ya Farid Musa.

Samatta amefanikiwa kuitunzia Tanzania rekodi dhidi ya Chad, kwani mara ya mwisho Taifa Stars alikutana na Chad, ugenini na kufanikiwa kuibuka kwa ushindi wa goli 2-1. Magoli ya Taifa Stars wakati huo yalifungwa na Mrisho Ngassa dakika ya 11 na Nurdin Bakari dakika ya 88, huku goli la Chad la kufutia machozi lilifungwa na Mahamat Labbo dakika ya 12.
raaaa
Msimamo wa Kundi G ulivyo hadi sasa
Taifa Stars itarudiana na Chad Jumatatu ya March 28 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, huku ikiwa imebakiza mechi mbili dhidi ya Nigeria ugenini na timu ya taifa ya Misri utakaochezwa uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.


Mtangazaji wa Clouds FM, Diva amesema Chidi Benz atamsaidia kuandika mashairi ya wimbo wake mpya alioupa jina ‘Kosa Langu.’

Kupitia Instagram, Diva amedai kuwa Mr Blue pia atahusika kwenye wimbo huo mpya unaovunja kimya chake cha zaidi ya miaka miwili kwenye muziki.

“@lamarfishcrab vibin this weekend , Nilikutana na Chid Benz Juzi, akaniahidi kuniandikia wimbo na Kusisitiza ndani ya Mwezi huu nifanye RNB Moja amazing,” ameandika Diva.

“Sometimes kuimba inahitaji hisia sana, hapa kati nimekubwa na misukosuko ya Mapenzi nikaumia sana , and i said why nat Put this into a love song … yes nikapata melody and the verse and chorus Paw jus like that .. called Lamar like YOH ‘ ts about time .. lets jus do the hook up, am very comfy when it comes to studio session with Lamar , matter fact ts been a while and me and blue this year tulikaa and discuss the return,” ameongeza.

“Then nikaanza andika , wimbo wangu verse ya Kwanza nimeandika Mwenyewe , Verse ya Pili itaandikwa na Chidi Benzi and Mr Blue Bayser atamalizia Na Rap Music , strictly RNB ‘ Leo usiku tunaanza kazi ya Kurekodi wimbo Unaitwa ‘ Kosa Langu ‘ saa 6:15 usiku , Production ya Fishcrab Cook Out. Utakuwa ni wa Kiswahili kilichounganika na kiingereza, a very beautiful song wish muuskize and Utatoka week 2 Mbele, after a week itakuja video then …

kuusambaza All over Africa , so stay Tuned, always been a fan of Chidi and Mr. Blue, Very Talented…. But Kosa Langu is jus tooo emotional , huwezi amini i crieeed wakati naandika , trials and tribulations , love this and that but sucha happy song , Extremely.”

“I believe in Chiddi Benz Chuma, I believe in his Talent as well , amenisisitiza sana Kufanya this song .. and y’all kno me i live it to the fullest and always givin a shot .. i live to Please My heart … And wanna Be Happy man, Music is the way forward ya Happiness , This time hits me to the core .. and i can’t deny it ama go with The flow YO… lemme.”

Kabla ya hapo Diva aliwahi kuachia wimbo Piga Simu aliomshirikisha Diamond na Mgonjwa kwa raha zako aliomshirikisha Mr Blue.



KUFURU! Mama wa staa mwenye jina kubwa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’, Sanura Kasimu ‘Sandra’ amedaiwa kufanya kufuru ya aina yake kwa kununua mtaa mzima, Tandale-Uzuri jijini Dar na kuikarabati nyumba yake aliyokuwa akiishi zamani kwa kutumia takriban shilingi 100 Milioni

Chanzo chetu makini ambacho kilifuatilia ishu nzima tangu nyumba hiyo ilipoanza kukarabatiwa, kimesema kwamba kwa kipindi kirefu ‘bi mkubwa’ huyo amekuwa akifika nyumbani hapo asubuhi na kuondoka jioni akisimamia ujenzi sambamba na binti yake, Esma.


 Nyumba hiyo kabla ya kukarabatiwa.


“Mama Diamond noma, kateketeza shilingi milioni 100 na bado nasikia ameshafanya mchakato wa kununua nyumba za jirani ili mtaa mzima uwe wao,” kilisema chanzo chetu.

Chanzo hicho kimezidi kutiririka kuwa mama Diamond anataka kuifanya nyumba hiyo kuwa bora zaidi kwani mbali na kuiboresha, kuna mpango wa kutengenezwa swimming pool (bwana la kuogelea).

 Ikiwa inakarabatiwa


Mara baada ya kupenyezewa ubuyu huo, gazeti hili lilifika kwenye nyumba hiyo na kuzungumza na mama Diamond aliyekuwa bize kusimamia ujenzi.



“Jamani! Taarifa hizi mmezitoa wapi tena? Kweli nimekarabati nyumba yetu iwe bora zaidi. Hayo mambo ya gharama na mipango mingine ni siri labda mje mmuulize Diamond akirudi Marekani lakini ukarabati huu mnaouona ndio nimeusimamia mimi na mwanangu Esma,” alisema mama Diamond.
Imekuwa Kama Kawaida kumsikia Roma akiiba Nyimbo za Siasa Lakini leo Hii kaja na Hii Bonge la Wimbo wa Mapenzi Hivi ulikuwa unajua kama Roma anajua Kubembeleza.

 Hebu fanya kuusikiliza hapa Wimbo wake Mpya
 Song _ Mtoto wa kigogo

Welcome to My Blog

Popular Post

Blogger templates

About views Blogger

Mrembo wetu wa leo

KONA YA KIJANJA YA KUJIDA VIA SNAPS

Powered by Blogger.

MY HOT BROGGER TZ

Like My Facebook Page

FOLLOW ME ON TWITTER

Contact Form

Name

Email *

Message *

- Copyright © TIMOKUCHAZ -Robotic Notes- Powered by Blogger - Designed by Johanes Djogan -