Showing posts with label NEWS. Show all posts



Moja ya gumzo kwenye mitandao ya kijamii kwa sasa ni uwepo wa video fupi inayomuonesha mwananke anayedaiwa kuwa mchawi baada ya kukutwa katikati ya barabara akiwa bila ungo na baadhi ya vitu vinavyodhaniwa vya kishirikina.
Sasa new stori leo leo July 20, 2017 kwenye Hekaheka ya Leo Tena ya Clouds FM mtangazaji Geah Habibu katusogezea hii iliyotokea Kipunguni ambako mwanamke mmoja mwenye mume na watoto alikutwa katikati ya barabara akiwa bila nguo kwa kinachodaiwa ni maelekezo ya Mganga.
Tukio hilo limetokea July 18, 2017 majira ya saa sita mchana ambapo baada ya kukutwa katika hali hiyo wananchi walidhani ni mchawi na wakadhamiria kumchoma moto lakini aliokolewa na Polisi baada ya taarifa kumfikia Mwenyekiti wa eneo hilo…sikiliza full stori kwa kuplay hapa!!!

Moja ya headlines zinazomuhusu mwimbaji sataa wa Bongofleva kutoka kundi la Yamoto Band, Beka Flavour leo July 20, 2017 ni kuhusu kushikiliwa kwake na Jeshi la Polisi DSM kwa mahojiano yaliyodumu kwa saa Tisa kuanzia saa tano Asubuhi hadi saa mbili Usiku.
Ayo TV na millardayo.com zimempata Beka Flavour>>>”Nipo hapa tangu saa tano Asubuhi kwamba natuhumiwa kutapeli pesa za jamaa mmoja kupitia mitandao yangu ya kijamii. Huyu jamaa anaishi Kigoma na anadai kuwa alikuwa akizungumza na mimi na anasema hakuwahi kuonana na huyo Beka basi nilipata taarifa a kuripoti katika kituo hiki na niliporudi kutoka Safari ndio nimelifika hapa.
“Nimetoka kwa dhamana na kikubwa ningependa kuwaomba watu na mashabiki wengi kwamba watu wanaotumia majina yetu sio kitu kizuri kwani kama huyo wa Kigoma aliyetuma pesa anadai ametuma zaidi ya milioni 8. Kwa hiyo, wawe makini na mitandao feki kwani Maromboso, Enoki na wengine hatuna kurasa za Facebook.” – Beka Flavour.
“Kwa sasa nina Manager mpya mbali na Yamoto Band” – Becka Flavour…PLAY kwenye hii VIDEO kutazama kila kitu!!!

Walichokizungumza Star TV baada ya kufungiwa na TRA

Thursday, 13 July 2017
Posted by Unknown
Tag :
Mapema leo kulikuwa na stori kuwa TRA Mwanza imeifungia Kampuni ya Sahara Media inayomiliki Star TV, RFA na Kiss FM wakiidai malimbikizo ya kodi ya zaidi ya Tsh. Bilion 4 wakiitaka kulipa ndani ya siku 14 vinginevyo kampuni itapigwa mnada.
Baada ya taarifa hizo Meneja Rasilimaliwatu wa Sahara Rafaeli Shilatu amekiri kufungiwa akidai ni kutokana na malimbikizo ya kodi baada ya uwekezaji mkubwa waliofanya wakati wa kuhama kutoka analogy kwenda Digital ingawa wanajitaidi kuhakikisha kwamba wanarudi hewani na kulipa kodi kama kawaida.
>>>”Lazima tukiri kwamba mmeshuhudia TRA wamefunga maeneo yetu ya kazi na hii inatokana na malimbikizo ya kodi ambayo siyo ya sasa ni ya muda mrefu hata nyie waandishi wa habari mnajua kwamba kadri uwekezaji unavyokuwa mkubwa ndivyo gharama zinazidi kwenye uwekezaji. So, ilitulazimu kutafuta fedha kwenye mabenki ili tuweze kukidhi matakwa ya Serikali ya kuhama analogy kwenda Digatal.
“Niwatoe wasiwasi Watanzania na wapenzi wa Sahara hili ni jambo la muda lakini kampuni yetu inafanya jitihada kuhakikisha kwamba haya yanamalizika vyombo vyetu virudi hewani.” – Rafaeli Shilatu 
Bonyeza Play hapa chini kusikiliza Full story. Source http://millardayo.com/
Welcome to My Blog

Popular Post

Blogger templates

About views Blogger

Mrembo wetu wa leo

KONA YA KIJANJA YA KUJIDA VIA SNAPS

Powered by Blogger.

MY HOT BROGGER TZ

Like My Facebook Page

FOLLOW ME ON TWITTER

Contact Form

Name

Email *

Message *

- Copyright © TIMOKUCHAZ -Robotic Notes- Powered by Blogger - Designed by Johanes Djogan -