Picha 60 za uzinduzi wa movie mpya ya KAJALA inayoitwa MBWA MWITU

Thursday, 25 September 2014
Posted by Unknown
Tag :

1 

2 

3 

4 

 5 

6 

7 

 IMG_5101 

 IMG_5122 

 IMG_5123 

IMG_5139 

IMG_5152 

IMG_5154 

IMG_5166 

 IMG_5169 

 IMG_5170 

IMG_5171 

IMG_5172 

 IMG_5174 

 IMG_5178 

 IMG_5179 

 IMG_5181 

 IMG_5184 

 IMG_5194 

IMG_5199 

IMG_5201 

 IMG_5202 

 IMG_5205 

IMG_5207 

 IMG_5211 

IMG_5213 

 IMG_5215 

IMG_5221 

IMG_5225 

IMG_5226 

IMG_5230 

IMG_5231 

 IMG_5234 

 IMG_5238 

 IMG_5241 

 IMG_5255 

 IMG_5260 

 IMG_5261 

 IMG_5263 

IMG_5267 

IMG_5272 

IMG_5273 

IMG_5274 

IMG_5283 

IMG_5296 

 IMG_5300 

 IMG_5307 

IMG_5312 

 IMG_5316 

 IMG_5319 
 
IMG_5320 

  IMG_5322 
 
IMG_5327 

  IMG_5329
Hili tukio Ni la mwaka kulishana Keki Kama Wanafanya yaoooo Ha Wametisha sana




 Dj Celvin Alipiga Ngoma kali Hadi watu wakasahau kilichawapeleka pale Haaaaa Kweli Rombo ina vipaji

 Hanc Kiumbe Mc Akiwa na watoto wakali Juddy & Mrs Van Baba la baba Pembeni Na miwani kama Saibogi


Sasa Hapa Usipime Maana Alijuta Kuwaalika Team Kulowesha Noooooooma 


 Happy Bithday tooooooooooU  Happy Bithday tooooooooooU   Happy Bithday tooooooooooU    Happy Bithday Dear Van  Happy Bithday to UUUUUU.......Ndio Nyimbo iliyokuwa inaimbwa kwa wakati huo


 Wana jiandaa kukata Keki


 Hii ndio Keki Yenyewe 


 Huyu sasa Ndio Mkata Keki Juddy     A.k.A ............... Ni follow Instagram nitakuambia @Timokuchaz


 Mama Mlezi Wa Van Jackson Huyu Hapa Akilishwa Keki Hatareeee


Ha haaa Nkwambie au Nikuchunie ili na wewe Siku nyingine Unifate Kwenye Party.................

Anasema Keki Ni Chungu Sanaaaaaaaaaaaaaaaa hahaaaahaaaaa Vino Muongo


 Sasa Hapa Mtoto Van Anarembwa Kweli Juddy Alipania Haaaaaaaaa

 Kasaloo Jr De LuNz Akimmwagia Shampeen baada tu ya Kuifungua



 Mtu wangu wa Nguvu Aliye Piga Picha Kushoto Kulia Pale Ni Toto BAya Haji Mabovu nae Hakuwa Nyuma Tuliluka Nae Pande Zile






Kwa Habari za haraka like page zetu    




mpira
Hii ni stori ambayo inaelekea kugusa zaidi mambo ya ndani ya kifamilia ambayo yapo baina ya mama mzazi wa Peter Manyika pamoja na Peter Manyika mwenyewe,baada ya mama mzazi kusikika Peter Manyika nae amevunja ukimya.

Simu alipopigiwa Peter Manyika ambaye hakujua kama Soudy Brown yuko na mama yake live studio alianza kwa kusema kuwa wako sawa lakini aliposikia sauti ya mama yake akiwa na Soudy alimuomba Soudy amtafute ili waongee.
87.8 Clouds Fm inasikika ukiwa Mbeya.
Bonyeza play kusikiliza.

 
DA! Duniani kuna mambo jamani! Katika hali isiyo ya kawaida, maeneo ya Tandale Kwatumbo jijini Dar, waombolezaji hawakuamini macho yao wakati walipomuona ‘marehemu’ Mohamed Salum ‘Fido’ (29) (pichani), akirejea nyumbani hapo huku maandalizi ya mazishi yake yakipamba moto na waombolezaji, hasa mkewe, mtoto na ndugu wakilia kwa uchungu kufuatia ‘kifo’ chake.

Tukio hilo la aina yake lilitokea Septemba 12, mwaka huu, saa sita mchana wakati shughuli mbalimbali za mazishi yake zikiendelea zikiwa ni pamoja na maandalizi ya chakula cha mchana kwa waombolezaji.

Iko hivi; Fido ni dereva wa bodaboda, kijiwe chake kikiwa Lumumba Mnazi Mmoja, Dar. Inadaiwa kwamba Septemba 10, mwaka huu alikamatwa na polisi wa ‘Tigo’, Lumumba kwa madai ya kutokuwa na kibali cha kuingia mjini, akapelekwa Kituo Kikuu cha Polisi (Central).

Pale kituoni, habari zinadai maafande hawakumruhusu kumpigia simu mkewe ili kumweleza yaliyompata, ndipo ndugu walipoamua kumtafuta kwa siku mbili bila mafanikio.

Septemba 11, mwaka huu, mkewe, kaka yake na baba yake mzazi walikwenda Hospitali ya Mwananyamala na kuingizwa chumba cha kuhifadhia maiti (mochwari) ambapo walioneshwa maiti moja! Vilio vikaibuka kwani wote walisema ni Fido. Marehemu huyo aliuawa kwa kugogwa na kitu kizito kichwani na maiti yake ilipelekwa hapo na polisi.

Ndugu hao walitoka na vilio hadi nyumbani na msiba ukawekwa kwa kukusanya mikeka na chakula kuanza kupikwa huku sehemu ya kuzikia makaburini ikitafutwa achilia mbali sanda kupatikana huku ndugu walio mbali wakijulishwa kuhusu msiba huo.

Siku ya tukio, watu wakiwa katika maandalizi ya mwisho kabla ya kuufuata mwili, ndipo Fido alipoibuka na kusababisha tafrani kubwa.Baadhi ya watu waliingia mitini kwa woga huku ndugu wakishangaa iweje maiti itoke mochwari yenyewe? Ndipo Fido alipotangaza kwa sauti kuwa, hakufa, alikuwa polisi.

Akizungumza na Uwazi huku akifakamia msosi kwa madai kuwa hakula tangu alipokamatwa, Fido alisema alikamatwa na polisi lakini akakosa njia ya kuwasiliana na familia yake.
Naye mke wa marehemu alipopewa nafasi ya kusema alikuwa na haya:

“Nimepigwa butwaa, siamini kama ndiye huyu mume wangu, watu wamekusanyika kwa ajili ya maombolezo, nilijua hatukonaye tena. Ama kweli Mungu mkubwa, nimefurahi kufika kwake nyumbani.
“Ilikuwa Jumatano saa 1.45 asubuhi mume wangu aliniaga na kwenda kazini kwake lakini hadi saa mbili usiku alikuwa hajarudi na si kawaida yake, ilikuwa nikipiga simu yake inaita tu.

“Ilibidi niende Tandale wanakohifadhia pikipiki, nilikuta wenzake wamesharudisha pikipiki lakini yeye alikuwa bado.“Tulifuatana na ndugu zangu hadi Lumumba hatukumuona, tulienda Kituo cha Polisi Msimbazi, Central, Oysterbay na Kawe lakini walituambia hakuna mtu mwenye jina hilo aliyekamatwa ama kupatwa na tatizo, ilibidi twende Hospitali ya Mwananyamala mochwari kuulizia kama kuna maiti iliyookotwa.

“Uongozi wa mochwari ulitueleza kuna maiti tatu zilizopelekwa na polisi lakini hazifahamiki, moja ni kwa ajali ya pikipiki, mwizi kuuawa na wananchi na nyingine kuokotwa ufukweni mwa bahari ikiwa imefungwa kamba mikononi na kukatwa panga kisogoni.

“Mimi, baba pamoja na shemeji yangu tuliingia mochwari kuthibitisha. Tulipofika katika maiti iliyofungwa kamba na kukatwa panga kisogoni wote tulijiridhisha kuwa ndiye yeye kutokana na alama alizokuwa nazo, sikujua kilichoendelea, naamini nilipoteza fahamu baada ya kuuona mwili huo.

“Tulirudi nyumbani kuandaa msiba, kuweka maturubai, kununua sanda na kuandaa jeneza, tulipiga simu sehemu mbalimbali hadi mikoani kuwajulisha ndugu.“Tulijiandaa ili ndugu wa Morogoro na mikoa mingine wakija katika mazishi yaliyotarajiwa kufanyika kesho Ijumaa (iliyopita) katika makaburi ya hapa Tandale ambapo tulishapewa eneo la kuchimba kaburi.

“Kweli sijui nisemeje, tuliwataka radhi waombolezaji kwa usumbufu, baadhi walitawanyika kwa wakati huo wengine waliendelea kuwepo hata ndugu zetu wengine wako njiani wakitokea Mbeya na Mtwara.”

2




Thanks Watu wangu wa Nguvu Najua bila Nyinyi nisinge Fika hapa. Mwanzo nilianza kama utani ila leo hii Naoana Mnanipa Moyo Leo Hii naomaba niwatambulishe Blogger Yangu Kuchaz.blogspot.com  

Naweza nikasema  1).Hii yote Nimeifanya kwa Msaada Wa kaka Angu Mpendwa Alico Shimwela Naweza kusema Bila yeye Nisingeweza Chochote Sina la Kusema Zaidi Ya asante Kaka Big Up Mungu Akupe Moyo Huo Huo Pia Akuppe Maisha Marefu 

2).Mdogo  Angu   Haji Mabovu  Aise Saruuuut Sana Mkuu Pale Nilipokuomba kitu Hukushindwa kunisaidia Mungu Akubariki Na akupe Akili za Ziada za kubuni na Kufanya Mambo makubwa Kuliko hayo unayoyafanya Asante  

3) Na Mwisho Ni wewe Ambae Ulipofungua na kusomasoma Yaliyomo Hukuchoka ukazidi Kunifatilia siku hadi Siku Hadi leo hii Blog Imefunguliwa na watu 1,00,00 Na sema Asanteni Nyote 

Mzidi Kuwa na Moyo 
 Huo Huo Zaidi Niseme Kitu Kama unaona Kuna sehemu nimekosea Please Usiache Kuniambia My No +255713624383 au +255753751970

 




 



Habari nzuri kwa wadau wa burudani ni kwamba Mkubwa na wanawe Wanamtambulisha msanii kutoka katika kituo chao  cha MKUBWA NA WANAWE na huyu msanii anakwenda kwa jina la Amir na huu hapa ni wimbo wake ambao unakwenda kwa jina la  NIKUPETI PETI Sikiliza na Download ngoma hiyo hapa na mpe support kijana huu kwa kila hali.
Salute pia kwa Team Mkubwa na Wanawe kwa kuendelea kuzalisha vipaji vyenye uwezo mkubwa wa kuandika mashairi na kutumia vizuri sauti zao na kutupa Burudani. Kumbuka Mkubwa na wanawe pia ndiyo imewaletea Yamoto band Wanaofanya poa kupitia ngoma yao kama Yamoto, Nibemende na Wimbo wao mpya unaokwenda kwa jina NISEME NISISEME

Ripoti nzima ya mchezo wa Yanga vs Azam FC hii hapa

Sunday, 14 September 2014
Posted by Unknown
Tag :



IMG_7230.JPG

Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Brazil Geilson Santos “Jaja” leo amewaonyesha wapenzi wa soka nchini nini kazi yake uwanjani baada ya kuisadia Young Africans kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 huku yeye akikwamisha mabao mawili safi mchezo uliofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa jijni Dar es salaam.
Young Africans ambayo ilikua ikicheza mchezo wa Ngao ya Jamii mbele ya mashabiki wake zaidi ya elfu thelathini waliofurika kuwapa morali wachezaji, walitulia na kucheza soka tangu mwanzo wa mchezo mpaka mwisho.
Kocha Mbrazil alianza na mfumo wa 4-5-1 walinzi Juma Abdul Oscar Joshua, Kelvin Yondani na Nadri Haroub “Canavvaro”, mbele yao wakicheza viungo wa Ulinzi Mbuyu Twite na Said Juma “Makapu” wakisaidiwa na Haruna Niyonzima, Mrisho Ngasa na mbrazil Jaja akianza mshambuliaji peke yake.
Kipindi cha kwanza kilianza kwa kasi kwa timu zote kusaka bao la mapema, mipira mirefu ya Mbuyu Twite kwa Mrisho Ngasa haikuwa na madhara sana langoni mwa timu ya Azam katika dakika 10 za mwanzo.
Kiungo Said Juma “Makapu” alikosa nafasi ya kuipatia Young Africans bao la kwanza dakika ya 10 baada ya mpira wa kona uliopigwa na Niyonzima, huku Nizar Khalfani pia akikosa kuifungia pia timu yake bao baada ya shuti la faulo alilopiga kutoka mita chache pembeni mwa lango la Azam.
Young Africans iliendelea kulishambulia lango la Azam FC kupitia kwa washambuliaji wake Geilson Santos “Jaja” Mrisho Ngasa na Nizar Khalfani lakini kutoku makini kulipelekea timu zote kwenda mapumziko zikiwa sare ya kutofungana.
Kipindi cha pili Young Africans ilianza kwa kufanya mabadiliko ambapo kocha aliwaingiza Hassan Dilunga na Saimon Msuva waliochukua nafasi za Said Juma na Nizar Khalfani hali iliyopelekea kikosi cha mbrazil Maximo kutawala eneo la kiungo.
Dakika ya 58 Geilson Santos “Jaja” aliwainua vitini mashabiki, wapenzi na wanachama wa klabu ya Young Africans baada ya kuipatia timu yake bao la kwanza katikati ya walinzi wawili wa Azam FC akiitumia vizuri pasi ya Saimon Msuva.
Geilson Santos “Jaja” dakika ya 66 ya mchezo aliwainua tena vitini washabiki, wapenzi na wanachama baada ya kufunga bao la pili kwa ufundi wa hali juu, baada ya kupenyezewa pasi nzuri na kiungo Hassan Dilunga na Jaja kuukota kwa hatua moja na kisha kumchambua mlinda mlango wa Azam FC Mwandini Ali kwa kuunyanyua kwa ufundi na kuamsha shangwe na nderemo uwanjani.
Huku wapenzi wa soka wakidhania mpira umemalizika, Saimon Msuva alimaliza ndoto za timu ya timu ya Azam kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kuipatia timu yake bao la tatu na ushindi na kuifanya Young Africans kuchukua Ngao ya Jamii kwa mara ya nne tangu kuanzishwa kwake huku Simba wakiwa wamechukua mara mbili na Mtibwa Sugar mara moja.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Young Africans 3 – 0 Azam FC.
Mara baada ya mchezo huo kocha mkuu wa Young Africans mbrazili Marcio Maximo amesema anawashukuru wachezaji wake kwa kucheza kwa kufuata maelekezo yake hali iliyoplekea kucheza soka safi la kuburudisha linaloambatana na ushindi.
Aidha Maximo amesema baada ya ushindi wa leo maandaliz ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar yataanza siku ya jumanne ambapo kwa kesho ametoa mapumziko kwa wachezaji wote pamoja na benchi la Ufundi.
Mwisho Maximo amewapongeza vingozi, waachezaji na washabik wa Young Africans kwa sapoti wanayoitoa kwa timu na kuomba wajitokeze kwa wingi pia mjin Morogoro mwishoni mwa wiki katika mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar.
Young Africans: 1. Deo Munish “Dida”, 2. Juma Abdul, 3.Oscar Joshua, 4. Nadir Haroub “Cananavao” (C), 5.Kelvin Yondani, 6.Mbuyu Twite, 7.Said Juma “Makapu”/Hassan Dilunga, 8.Haruna Niyonzima/Hamis Kizza, 9.Geilson Santos “Jaja”/Hussein Javu, 10.Mrisho Ngasa/Omega Seme, 11.Nizar Khalfani/Saimon Msuva/
Azam FC: 1.Mwadini Ali, 2.Shomari Kapombe, 3.Erasto Nyoni/Gadiel Michael, 4.David Mwantika, 5.Agrrey Morrsi, 6.Kipre Balou, 7.Himid Mao/Kelvin Friday, 8.Salum Abubakar, 9.Didier Kavumbag, 10.Kipre Tchetche/Ismail Diara, 11.Leonel st.Pres/Khamis Mcha
Source: Yanga official website

Kuna Wadada Wamebariki Makalio, Embu Ona Hii Video Fupi Huyu Dada anayejiita Irene Anavyotingisha Wezele Lake Huku Akijiangalia Kwenye Kioo cha Meza ya Kujirembea..Shidaa Tupu:
 

Sipendi Watu Wanavyoniambia Nina Kalio Fake, Wakati Nimebarikiwa na Mungu

 
Admin , Sipendi Jinsi watu wanavyonisema kila nipitapo eti makalio yangu ya Mchina wakati mimi nimezaliwa hivyo hivyo toka nikiwa mdogo makalio yangu yalikuwa makubwa , kama unabisha uliza hata nilio soma nao shule ya msingi , Ki kweli sipendi hiyo tabia ya watu kila wakiona mtu amejaliwa basi eti ni fake wengine tumezaliwa hivyo jamani ..Khhaa  

Kama Ulikua huja like Page yetu 

Welcome to My Blog

Popular Post

Blogger templates

About views Blogger

Mrembo wetu wa leo

KONA YA KIJANJA YA KUJIDA VIA SNAPS

Powered by Blogger.

MY HOT BROGGER TZ

Like My Facebook Page

FOLLOW ME ON TWITTER

Contact Form

Name

Email *

Message *

- Copyright © TIMOKUCHAZ -Robotic Notes- Powered by Blogger - Designed by Johanes Djogan -