Video queen ambaye haishiwi vituko, Gigy Money amefunguka kwa kusema
kuwa yeye siyo mtu wa kupenda kufanya mapenzi kama watu wanavyodhani.
Akizungumza na Bongo5, Gigy amesema maisha aliyopitia yamemfanya awe ni mwanamke asiyependa kufanya mapenzi.
“Mimi nimepoteza ile ari ya kufanya mapenzi au kuwa na mpenzi mmoja au
nijiachie na mwanaume kama mtu na mpenzi wake siwezi, sasa hivi natafuta
maisha, pesa mbele,” alisema Gigy. “Kama yeye ana wivu na mimi, mimi
sina wivu na mwanaume,”
Gigy amesema taarifa za kwenye mitandao ya kijamii kwamba anajiuza siyo
za kweli, kwani yeye ana mwanaume ambaye anamuudumia kila kitu ingawa
hawafanyi mapenzi.
“Nina mtu ambaye ananihudumia, ananipa mtaji ya biashara zangu. Pia hata
kwenye muziki anawekeza pesa yake. Kwa hiyo waache wanifikie hivyo
wanavyofikiria, mimi nafikiria navyojijua, mimi nipo tofauti sana na
wanavyozungumza, ukijaribu kukaa na watu wangu wa karibu watakwambia,”
alisema Gigy.