Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk
John Pombe Magufuli, April 5 2016 jina lake limerudi kwenye headlines kwa mara nyingine tena. Rais
Magufuli amerudi kwenye headlines baada ya kukubali mwaliko wa Rais
Paul Kagame wa
Rwanda, hivyo atafanya ziara ya siku mbili Jumatano na Alhamisi.
Stori kutoka wizara ya mambo ya nje zinaeleza kuwa Rais
Magufuli pamoja na Rais
Kagame watafungua daraja la kimataifa la
Rusumo linaounganisha mpaka wa
Tanzania na
Rwanda
na kuzindua ushirikiano wa huduma za kituo cha pamoja.Kwa mujibu wa
taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari na kusomwa katika television
za
Tanzania Rais
Magufuli atasafiri kwa gari.
Kutoka kushoto ni Rais Magufuli na Rais Paul Kagame wa Rwanda
Rais
Magufuli pia atakwenda kuweka shada katika makaburi ya mauaji ya Kimbali ya mwaka 1994 na baadae kufanya mazungumzo ya pamoja na Rais
Kagame mjini
Kigali. Hii ndio itakuwa safari ya kwanza ya Rais
Magufuli kusafiri nje ya nchi toka aingie madarakani October 2015.