Najua Ulimiss sana Kuisikia Sauti ya FEROOZ..Sasa amekuletea bonge la
Ngoma akiwa chini ya MKUBWA FELLA , Hii ngoma ameshirikiana na RAYMOND
kutoka kwa Wasafiii .... Ngoma Hii HAPA ipakueee Mkali wangu
This song"FREEDOM"Has Been Produced By Daxo Challi (MJ RECORDS) From
Tanzania And Written By SUGU 'The Video Was Directed By Hanscana from
Wanene Films.
Ukiona umemtumia mpenzi wako/mchumba wako/mchepuko wako/mke wako au hata
rafiki wa kike wakati mwingine SMS ya kawaida tu kwaajili ya kumsalimia
lakini yeye akakujibu moja kati ya majibu yafuatayo, tafadhali sana
usiendelee kuchat nae maana kinachofuata hapo ni majanga tu.
KWA MFANO:
1. Ukimtumia sms ''Mambo mpenzi wangu?'' akikujibu ''mambo mabaya'',
usimuulize kwanini mambo mabaya, ukimuuliza atakwambia kuwa ''sina hela
dear''
3. Ukimtumia sms ''Mbona kimya sana mchumba wangu, umenitupa kiasi
hicho'' akikujibu ''sijakutupa wangu yaani mambo hata hayaendi''
usimuulize kwanini mambo hayaendi, ukimuuliza atakwambia kuwa ''yaani
sina kitu mpenzi wangu, simu ilikuwa haina hata hela ya kubeep''
4. Au ukiona mwanamke anaanza kwa kukwambia nikwambie kitu? We mkatalie
kiutani utani tu, mwambie usiniambie, hata akikomaa vipi akwambie
mwambie sitaki uniambie huku unafanya kama utani lakini moyoni unakuwa
upo serious.
Ni mara chache sana mwanamke akikwambia kuwa mambo mabaya, maisha magumu
au mambo hayaendi huwa na matatizo mengine kama kuumwa, misiba.... n.k
lakini THE REST ni wapigaji mizinga tu. Akikwambia maisha magumu mjibu
''pole wangu, mambo mengine vipi?''
Ukipewa majibu kama hayo, chagua moja, either usiendelee kuchat nae
mpaka badae kidogo au mbadilishie maada ili kukwepa huo mzinga ambao
unakuja mbele yako.
Lady Jaydee ametoa maana ya wimbo wake ‘Ndindindi’ ambalo lilikuwa
ni fumbo lililokuwa linawapa majibu mengi yasiyokuwa na uhakika
mashabiki wake.
Wimbo wa ‘Ndindindi’ unazidi kufanya Vizuri kwenye medi mbalimbali na
kumrudisha vizuri Jide aka Binti Komando kwenye muziki wa Bongo Fleva
baada ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila ya kuachia wimbo wowote.
Akiongea kwenye kipindi cha FNL, kinachoruka kupitia EATV, Lady
Jaydee alisema, “The Ndi mimi ni kitu tori wewe si kitu” lakini pia
aliongezea “ili kuleta fleva ya muziki ndiyo nikaiita Ndindindi. Mimi ni
kitu na wewe si chochote.”
April 17 2016 Mkuu wa mkoa wa Dar es salaamPaul Makonda
alikutana na waandishi wa habari na kuzungumzia baadhi ya changamoto
zinazoendelea katika jiji lake ikiwa ni pamoja na vitendo vya matumizi
mabaya ya fedha yanayofanywa na baadhi ya viongozi, Makonda
anasema>>
‘Kwenye
mkoa wetu wa Dar es salaam tuna mambo ambayo yamekuwa yakiendelea
ambayo yamekuwa yakikiuka sheria, kanuni na taratibu, moja ya vitu
vilivyobainika katika stendi ya ubungo imebainika kwamba Meneja anatumia
sharia ya mwaka 2004 kulipa mapato, wakati sharia inayotambulika kwa
sasa ni sharia ya mwaka 2009’
‘Mkataba
wa mwaka 2009 kwa mwezi tunapaswa kukusanya si chini ya mil 84, wakati
wa mwaka 2004 tunakusanya mil 42 kwa mwezi, manaake tunapoteza mil 42
kwa mwezi’
‘Hapa
inamaana kwa mwaka ni zaidi ya Milioni 500 zinapotea, na ukiangalia
kuanzia mwaka 2009 tumepoteza jumla ya Bil 3, ajabu waliosaini mkataba
wa tarehe 30/01/2015 ndio walewale waliosaini tarehe 31/01/2015’
Lakini pia ishu ya maegesho ya magari haijampita Makonda, na anasema ‘Upande
wa maegesho ya jiji inaonekana mzabuni tenda yake ilikwisha muda wake,
chaajabu haikutangazwa tenda bali akaandikiwa barua ya kuongezewa muda,
jambo ambalo halipo kisheria’
‘Sasa hapa inaonekana kuna uhusiano mazuri sana kati ya wanaokusanya pesa na wale wanaopokea, na watu hao ni viongozi’
Vipi kuhusu ishu ya bodaboda? Makonda anasema ‘Faini
ya makosa ya pikipiki ni shilingi elfu 20, lakini Tambaza anawatoza
watu elfu 80, imefika hatua wanakatazwa kumkamata mtu bila kujieleza,
lakini kinachofanyika ni kinyume na taratibu’
‘Hawa
Wakurugenzi ambao ambao badala ya kutusaidia sasa wameamua
kutuangamiza, nimeiomba mamlaka husika ya nidhamu ichukue hatua stahiki,
mimi kwenye mkoa wangu siwahitaji kuendelea kuwanyonya wana Dar es
salaam’
Roma Mkatoliki ni
msanii maarufu wa hiphop Tanzania ambaye kwenye upande wa pili wa maisha
ameamua kufunga ndoa na mpenzi wake wa longtime ambaye wana mtoto
pamoja (Ivan) na April 9 2016 ndoa imefungwa nyumbani Tanga na ni baada ya send-off kufanyika Dar es salaam February 2016.
February 2016 kwenye send-off Roma Mkatoliki akisindikizwa na mshkaji wake Kala Jeremih. Hip Hop Tz
Huduma ya WhatsApp haitatumika tena katika simu zinazotumia mifumo kadha
ya programu ikiwemo Blackberry 10, Nokia Symbian S60 na Windows Phone
7.1.
Kampuni ya Facebook inayomiliki huduma hiyo imesema inataka kuangazia
kustawisha “huduma katika mifumo inayotumiwa na watu wengi.”
WhatsApp, itaacha kufanya kazi katika mifumo hiyo ya programu kufikia
Desemba 2016. Licha ya kuacha kutumika katika simu nyingi za Blackberry,
WhatsApp bado itaendelea kutumiwa katika simu za kisasa zaidi za
Blackberry kwa sababu simu hizo hutumia mfumo wa Android.
Kampuni hiyo imejitetea na kusema kwamba haijawatupa wateja wake ambao
wamechangia sana katika ufanisi wake lakini ni kutokana na mabadiliko ya
teknolojia.
“Simu hizi hazina uwezo wa kiteknolojia tunaohitaji kuendelea kuimarisha huduma yetu siku zijazo,” kampuni hiyo imesema.
Orodha kamili ya mifumo ya simu ambayo wateja hawataweza tena kutumia WhatsApp ni hii hapa: Android 2.1 and Android 2.2
Blackberry OS 7 and earlier
Blackberry 10
Nokia S40
Nokia Symbian S60
Windows Phone 7.1
Kampuni hiyo imesema wakati wa kuanzishwa kwa WhatsApp mwaka 2009,
asilimia 70 ya simu wakati huo zilikuwa za BlackBerry na Nokia.”
Lakini sasa asilimia 99.5 ya simu zinatumia mifumo ya Google, Apple na Microsoft.
Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Dk John Pombe Magufuli, April 5 2016 jina lake limerudi kwenye headlines kwa mara nyingine tena. Rais Magufuli amerudi kwenye headlines baada ya kukubali mwaliko wa Rais Paul Kagame wa Rwanda, hivyo atafanya ziara ya siku mbili Jumatano na Alhamisi.
Stori kutoka wizara ya mambo ya nje zinaeleza kuwa Rais Magufuli pamoja na Rais Kagame watafungua daraja la kimataifa la Rusumo linaounganisha mpaka wa Tanzania na Rwanda
na kuzindua ushirikiano wa huduma za kituo cha pamoja.Kwa mujibu wa
taarifa zilizotolewa na vyombo vya habari na kusomwa katika television
za Tanzania Rais Magufuliatasafiri kwa gari.
Kutoka kushoto ni Rais Magufuli na Rais Paul Kagame wa Rwanda
Rais Magufuli pia atakwenda kuweka shada katika makaburi ya mauaji ya Kimbali ya mwaka 1994 na baadae kufanya mazungumzo ya pamoja na Rais Kagamemjini Kigali. Hii ndio itakuwa safari ya kwanza ya Rais Magufuli kusafiri nje ya nchi toka aingie madarakani October 2015.
Van Jack a.k.a Arsene_Wenger wemgi ndivyo wanavyomuita hivyo pande za Ubungo jijin dar Tanzania Ni maarufu sana pande hizo hidi Snaps company Imeamua kumpa offer ya Picha Hii Unaweza ukamfollow kwa link hizi FacebookInstagram Kama na wewe Unahitaji utokelezee na Chama lako wasiliana nasi kwa
Binti akiwa na Shanga wazee wa zamani wanasema huyo ana adabu Hilo jambo kweli linamaana Japo sina uhakika Wadada wa Leo wanazitumia Vizuri hizo Shanga
Usichukue muda kujiuliza mara yako ya mwisho kutazama video mpya ya Mh. Temba ilikua lini? right now yuko kwenye spika zetu na hii single inaitwa ‘fundi’ na ukishatazama usisahau kuniachia comment yako hapo chini ili Temba akipita hapa ajue mashabiki wake wameipokeaje.
Mamlaka ya Usimamizi wa Huduma za Nishati na Maji EWURA imetangaza
kushusha bei za umeme kuanzia leo kwa watumiaji wote wa viwango tofauti.
Kushuka huko kwa bei ya umeme ni kutokana na ombi la Shirika la Umeme
Tanzania TANESCO kutaka bei za umeme zipunguzwe sambamba na hilo gharama
za huduma kwa baadhi ya wateja zimeondolewa.
Bei mpya kwa watumiaji wadogo ni sh.100 kwa uniti, watumiaji wa kati ni
sh.292 toka 298 ya zamani.Wafanyabiashara wadogo ni sh. 195 toka
sh. 200 ya hapo awali.
Bei mpya kwa wafanyabiashara wa kati ni sh.157 toka sh. 159. Wanaonunua
kwa wingi (bulk) ni sh. 152 toka sh. 156 ya hapo awali
Licha
ya jitihada za serikali kutangaza vita dhidi ya wauzaji na wanunuzi wa
miili ya kinadada na kuwataka waache kwa kuwa ni kinyume cha maadili na
sheria ya nchi, warembo hao (sio walio pichani ukurasa wa nyumawamedaiwa
kukaidi agizo hilo huku wakidai kama aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Yusuf Makamba alishindwa basi hata mkuu mpya wa mkoa huo, Paul
Makonda hatawaweza. Hivi
karibuni, Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, CP Simon Sirro
alitangaza oparesheni maalum ya kuwasaka madada poa hao, sambamba na
wateja wao akidai wanakiuka sheria na maadili ya Mtanzania jambo ambalo
liliungwa mkono na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto, Ummy Mwalimu. Mara
baada ya agizo hilo la serikali kutolewa, wanahabari wetu walifanya
uchunguzi katika maeneo ambayo yamezoeleka kwa biashara hiyo na kukuta
baadhi yao wakiendelea kama kawaida kana kwamba hakuna agizo lolote
lilitolewa. Risasi
lilipita maeneo ya Sinza-Mori jijini Dar na kuwakuta akina dada hao
wakiendelea na biashara hiyo kwa kujipanga barabarani kuelekea baa
maarufu ya Meeda ambapo wanahabari wetu waliojifanya wateja
walipowauliza kulikoni hawaogopi nguvu ya dola, walisema wao
wameshindikana tangu enzi za Makamba, Kandoro na Said Meck Sadick
(aliyepita) hivyo hata huyu wa sasa, Makonda hatawaweza. Wewe
hii ni nguvu ya soda. Hatuwezi kuacha unafikiri tutakula wapi? Hii kazi
tumeanza kitambo, tangu enzi za Makamba aliyekuwa hatari kweli kukemea
biashara hii lakini tulimshinda. Akaja Sadick naye tukamgaragaza sembuse
huyu Makonda aliyepewa jiji hili juzi tu?” alisema dada poa mmoja
aliyekataa kutaja jina lake. Maeneo
mengine ya Jiji la Dar ambayo Risasi lilibaini kuwa biashara hiyo bado
inaendelea kama kawaida ni pamoja na Sinza-Afrikasana (maarufu kama
Conner Bar), Buguruni (Kimboka Bar, Rozana), Temeke na
Kinondoni-Makaburini. Alipotafutwa
Makonda kuhusiana na suala hilo alisema atalizungumza kwa kirefu baada
ya Sikukuu ya Pasaka lakini mwanahabari wetu alipombana zaidi ili aweze
kutoa ufafanuzi kwa kuwa madada poa hao wamekaidi agizo la serikali,
aliahidi kulizungumzia siku iliyofuata (Machi 21) lakini hata hivyo siku
hiyo alipopigiwa simu hakupokea. Hata mwandishi wetu alipomtumia ujumbe mfupi wa maandishi kumsisitiza azungumzie suala hilo, Makonda hakujibu chochote. Aidha,
mwandishi wetu pia alimtafuta Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalum ya Dar
es Salaam, Simon Sirro ili aweze kuzungumzia suala hilo, aliomba
atafutwe baadaye kwa kuwa alikuwa kwenye kikao. Baadaye simu yake
haikupatikana hewani. GPL
Rais John Pombe Magufuli aliwateua wakuu wapya wa mikoa Tanzania bara March 13 2016 ambapo kati yao 13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, watano wamehamishwa
vituo vya kazi na mmoja amepangiwa Mkoa mpya wa Songwe sasa wakati wa
kuwaapisha kuna mmoja wa viongozi aliteleza kufata kanuni za viapo,
tazama kwenye hii video hapa chini.
Timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars March 23 imeshuka katika dimba la Idriss Mahamat kucheza na wenyeji wao timu ya taifa ya Chad katika muendelezo wa michezo ya makundi ya kuwania kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON) itakayochezwa mwaka 2017.
Huu ulikuwa ndio mchezo wa kwanza wa Mbwana Samatta akiichezea Taifa Stars kama nahodha wa timu hiyo, katika mchezo huo uliochezwa Chad, Taifa Stars imeibuka na ushindi wa goli 1-0, goli la Taifa Stars lilifungwa na Mbwana Samatta dakika ya 30, baada ya kutumia vyema krosi ya Farid Musa.
Samatta amefanikiwa kuitunzia Tanzania rekodi dhidi ya Chad, kwani mara ya mwisho Taifa Stars alikutana na Chad, ugenini na kufanikiwa kuibuka kwa ushindi wa goli 2-1. Magoli ya Taifa Stars wakati huo yalifungwa na Mrisho Ngassa dakika ya 11 na Nurdin Bakari dakika ya 88, huku goli la Chad la kufutia machozi lilifungwa na Mahamat Labbodakika ya 12.
Msimamo wa Kundi G ulivyo hadi sasa
Taifa Stars itarudiana na Chad Jumatatu ya March 28 uwanja wa Taifa Dar Es Salaam, huku ikiwa imebakiza mechi mbili dhidi ya Nigeria ugenini na timu ya taifa ya Misri utakaochezwa uwanja wa Taifa Dar Es Salaam.
Mtangazaji wa Clouds FM, Diva amesema Chidi Benz atamsaidia kuandika mashairi ya wimbo wake mpya alioupa jina ‘Kosa Langu.’
Kupitia Instagram, Diva amedai kuwa Mr Blue pia atahusika kwenye wimbo
huo mpya unaovunja kimya chake cha zaidi ya miaka miwili kwenye muziki.
“@lamarfishcrab vibin this weekend , Nilikutana na Chid Benz Juzi,
akaniahidi kuniandikia wimbo na Kusisitiza ndani ya Mwezi huu nifanye
RNB Moja amazing,” ameandika Diva.
“Sometimes kuimba inahitaji hisia sana, hapa kati nimekubwa na
misukosuko ya Mapenzi nikaumia sana , and i said why nat Put this into a
love song … yes nikapata melody and the verse and chorus Paw jus like
that .. called Lamar like YOH ‘ ts about time .. lets jus do the hook
up, am very comfy when it comes to studio session with Lamar , matter
fact ts been a while and me and blue this year tulikaa and discuss the
return,” ameongeza.
“Then nikaanza andika , wimbo wangu verse ya Kwanza nimeandika Mwenyewe ,
Verse ya Pili itaandikwa na Chidi Benzi and Mr Blue Bayser atamalizia
Na Rap Music , strictly RNB ‘ Leo usiku tunaanza kazi ya Kurekodi wimbo
Unaitwa ‘ Kosa Langu ‘ saa 6:15 usiku , Production ya Fishcrab Cook Out.
Utakuwa ni wa Kiswahili kilichounganika na kiingereza, a very beautiful
song wish muuskize and Utatoka week 2 Mbele, after a week itakuja video
then …
kuusambaza All over Africa , so stay Tuned, always been a fan of
Chidi and Mr. Blue, Very Talented…. But Kosa Langu is jus tooo
emotional , huwezi amini i crieeed wakati naandika , trials and
tribulations , love this and that but sucha happy song , Extremely.”
“I believe in Chiddi Benz Chuma, I believe in his Talent as well ,
amenisisitiza sana Kufanya this song .. and y’all kno me i live it to
the fullest and always givin a shot .. i live to Please My heart … And
wanna Be Happy man, Music is the way forward ya Happiness , This time
hits me to the core .. and i can’t deny it ama go with The flow YO…
lemme.”
Kabla ya hapo Diva aliwahi kuachia wimbo Piga Simu aliomshirikisha Diamond na Mgonjwa kwa raha zako aliomshirikisha Mr Blue.
KUFURU! Mama wa staa mwenye jina kubwa Bongo, Nasibu Abdul ‘Diamond
Platnumz’, Sanura Kasimu ‘Sandra’ amedaiwa kufanya kufuru ya aina yake
kwa kununua mtaa mzima, Tandale-Uzuri jijini Dar na kuikarabati nyumba
yake aliyokuwa akiishi zamani kwa kutumia takriban shilingi 100 Milioni
Chanzo chetu makini ambacho kilifuatilia ishu nzima tangu nyumba hiyo
ilipoanza kukarabatiwa, kimesema kwamba kwa kipindi kirefu ‘bi mkubwa’
huyo amekuwa akifika nyumbani hapo asubuhi na kuondoka jioni akisimamia
ujenzi sambamba na binti yake, Esma.
Nyumba hiyo kabla ya kukarabatiwa.
“Mama Diamond noma, kateketeza shilingi milioni 100 na bado nasikia
ameshafanya mchakato wa kununua nyumba za jirani ili mtaa mzima uwe
wao,” kilisema chanzo chetu.
Chanzo hicho kimezidi kutiririka kuwa mama Diamond anataka kuifanya
nyumba hiyo kuwa bora zaidi kwani mbali na kuiboresha, kuna mpango wa
kutengenezwa swimming pool (bwana la kuogelea).
Ikiwa inakarabatiwa
Mara baada ya kupenyezewa ubuyu huo, gazeti hili lilifika kwenye nyumba
hiyo na kuzungumza na mama Diamond aliyekuwa bize kusimamia ujenzi.
“Jamani! Taarifa hizi mmezitoa wapi tena? Kweli nimekarabati nyumba yetu
iwe bora zaidi. Hayo mambo ya gharama na mipango mingine ni siri labda
mje mmuulize Diamond akirudi Marekani lakini ukarabati huu mnaouona ndio
nimeusimamia mimi na mwanangu Esma,” alisema mama Diamond.
Imekuwa Kama Kawaida kumsikia Roma akiiba Nyimbo za Siasa Lakini leo Hii kaja na Hii Bonge la Wimbo wa
Mapenzi Hivi ulikuwa unajua kama Roma anajua Kubembeleza.
Habari kubwa Magazetini Kenya leo March 3, 2025
-
Good Morning Mtu wangu wa nguvu kutoka Tanzania March 3, 2025,nakukaribisha
kutazama kile kilichoandikwa katika kurasa za mbele na za nyuma Magazetini
ke...